Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume (kulia), akiendesha Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, kwenye Ukumbi wa CCM Kisiwandui, Mjini Zanzibar leo. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, akiendesha kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, kwenye Ukumbi wa CCM Kisiwandui, Mjini Zanzibar leo. Kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Dk. Ali Mohamed Shein na kulia ni Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai.
Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, (wa pili kushoto), Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, Balozi Seif Ali Iddi (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, kwa pamoja wakiwa wamesimama kabla ya kuanza kikao cha siku moja cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, kilichofanyika leo, Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, wakiwa katika kikao cha siku moja chini ya Mwenyekiti wake, Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kinachofanyika Ukumbi wa CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na kumpongeza Mwakilishi mpya wa Jimbo la Bububu CCM, Hussein Ibrahim Makungu (kulia), kwa kushinda uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui, Mjini Zanzibar leo, kushiriki katika Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, Kisiwandui.
Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, akisalimiana na kumpongeza Mwakilishi mpya wa Jimbo la Bububu CCM, Hussein Ibrahim Makungu (kulia), kwa kushinda uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, alipowasili katika viwanja vya Ofisi ya CCM Kisiwandui, Mjini Zanzibar leo, kushiriki katika Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya Zanzibar, kilichofanyika leo.

No comments:
Post a Comment