Meneja wa benki ya NMB, Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kulia), akipeana mkono na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Hekima, Buguruni, Manispaa ya Ilala, katika hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 yaliyotolewa na Benki hiyo jijini leo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Hekima, Buguruni, iliyopo Manispaa ya Ilala, wakifurahia madawati yaliyotolewa na benki ya NMB leo kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la uhaba wa madawati shuleni hapo. Msaada huo umetolewa siku moja kabla ya kuanza kwa mtihani wa taifa wa darasa la saba.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga (wa pili kushoto), akipeana mkono na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Salie Mlay (kulia), wakati wa makabidhiano ya madawati 50 yenye thamani ya sh milioni 5, jijini leo.

No comments:
Post a Comment