Sehemu ya Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), kutoka shule ya mafunzo na huduma Pangawe mkoani Morogoro, wakiweka taka ngumu katika lori, wakati wa zoezi la kufanya usafi ndani na nje ya Soko Kuu la Mkoa huo jana, ikiwa ni sehemu mojawapo ya kuadhimisha maadhimisho ya miaka 48 tangu kuanzisha kwa jeshi hilo, ambapo kilele cheke hufanyika kila Septemba Mosi kila mwaka hapa nchini.
Hapa askari hao wakiwa na tenga lenye uchafu wakielekea katika lori kwa ajili ya kutupa taka hizo.
Wakikusanya uchafu uliopo chini na kuweka katika vyombo.
Kazi hiyo iliendelea katika sehemu nyingine katika soko hilo kama wanavyoonekana askari hao wakiendelea na zoezi hilo.
Askari huyu akizoa taka ngumu kutoka chini na kuweka katika toroli baada ya kuzitoa ndani ya mtaro katika mtaa wa Uhuru unaopakana na Soko Kuu hilo.
Kwa kweli kazi zilikuwa nyingi sana hapa afande akisukuma toroli lenye taka hizo wakati akielekea kwenye lori la kukusanyia taka. (Picha na mdau wetu)







No comments:
Post a Comment