| Meneja Mauzo wa Kampuni ya Usambazaji wa kazi za sanaa msanii Mzee Yussuf 'MY Collection', Mussa Msuba akiwa katika duka la mauzo ya kazi za kundi la Jahazi, linaloongozwa na msanii Mzee Yussuf. |
Na Mwandishi Wetu
| DVD ZA JAHAZI |
| Meneja wa duka la MY, Msuba |
MSANII wa muziki wa Taarabu nchini Mzee Yussuf ameamua kuanzisha kampuni yake ya usambazaji kazi zake ijulikanayo kwa jina la MY Collection kwa ajili ya kusambaza kazi zake.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Meneja Mauzo wa Kampuni hiyo, Mussa Msuba amesema kuwa wameamua kufungua duka kwa ajili ya kuuza CD NA DVD za bendi ya Jahazi, inayongozwa na Mzee Yussuf.
Duka hilo lililopo makutano ya barabara ya Likoma na Muhonda linajihusisha na
kuuza DVD za taarabu kwa jumla na rejareja kwa ajili ya kuwaletea karibu wapenzi wake ili waweze kupata burudani kupitia nyimbo zao ili kuweza kupata burudani hata majumbani mwao.
Msuba amesema kuwa, Mzee Yusufu yupo mbioni kutoa albamu yake mpya ya mduara, itakayotoka hivi karibuni, ambayo anaitoa kivyake vyake, nje ya bendi yao ya Jahazi.
Amesema mbali na hilo, bendi hiyo itatoa video yake ya nyimbo zake za albamu zake zote za Two in One, Kazi ya Mungu, Nakula Naksh Naksh, Tupendane na Daktari wa Mapenzi.
Ambazo zitakuwa madukani kwa ajili ya kuwapa wapenzi wao burudani wakiwa majumbani mwao
Naye Mzee Yussuf, aliongeza kwa kusema kuwa ameanzisha Kampuni yake hiyo, baada ya kuona kwamba kazi zake nyingi zimekuwa zikichakachuliwa kutokana na kuwepo kwa wizi wa kazi za wasanii.
Msanii Mzee Yussuf ameanzisha duka hili, lililopo mtaa wa Muhonda na Likoma kwa ajili ya CD za Jahazi pekee. Mbali na duka hilo Mzee Yusufu anamiliki duka lingine la nguo lililopo Magomeni Mapipa kwa ajili ya kujiongezea kipato chake nje ya bendi yake.
Bendi ya Jahazi mpaka sasa imeshatoa albam zake nane ambazo zipo madukani hivi sasa.
Kwa sasa bendi hiyo ipo mbioni kuachia albamu yake ya tisa, ambayo hadi sasa haijapewa jina na inatarajiwa kuzinduliwa mwezi October mwaka huu.
Amewataka mashabiki wa kundi hilo kujiandaa kwa ajili ya kupata burudani kutoka kwa kundi hilo wakati wa uzinduzi wa album zake hizo.

No comments:
Post a Comment