TANGAZO


Sunday, September 9, 2012

Hafla ya uzinduzi wa Kambi ya Redd's Miss Kinondoni 2012, Dar es Salaam


Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni 2012, Vivien Sirikwa (kushoto), akiwatambulisha Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye (katikati) pamoja na Sebo ambaye ni mmoja kati ya mwakamati ya Redd’s Miss Kinondoni 2012, wakati wa uzinduzi wa kambi yao, ambayo ipo Hoteli ya JB Belmonte, jengo la Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye akizindua kambi ya Redd’s Miss Kinondoni 2012 jijini Dar es Salaam leo.  Mbele kulia ni Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni 2012, Vivien Sirikwa na nyuma ni warembo wa kinyang’anyiro hicho.

Mratibu wa Redd’s Miss Kinondoni 2012, Vivien Sirikwa akiongea mbele ya warembo hao, jijini Dar es Salaam leo. 

Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya JB Belmount, ambao ni wadhamini wa Redd’s Miss Kinondoni 2012, J. Baguma, akiongea katika uzinduzi wa kambi hiyo, iliyopo hotelini hapo.

Washiriki wa Kinyang’anyiro cha Redd’s Miss Kinondoni wakiwa katika picha ya pamoja, mara baada ya kuzinduliwa kambi yao leo.

Baadhi ya warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2012, wakiserebuka wakati wa uzinduzi leo.

Baadhi ya warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2012, wakiserebuka muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa uzinduzi huo leo.
Ilikuwa ni kuserebuka tu leo kwa warembo wa Redd’s Miss Kinondoni 2012, baada ya kuzinduliwa kambi yao jijini Dar es Salaam leo.

Mauno mpaka kesho hakuna kukaa kwa mamis hao.

No comments:

Post a Comment