TANGAZO


Wednesday, September 5, 2012

Chuo Kikuu Huria wazindua ujenzi wa Jengo Kuu la Elimu



Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly Mbwette, akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa  ujenzi wa Jengo Kuu la Elimu la chuo hicho, jijini Dar es Salaam leo. Uzinduzi huo, umeenda sambamba na uzinduzi wa kituo cha utawala bora kwa masomo ya Uandishi wa habari pamoja na uzinduzi wa masomo ya Kifaransa. Katikati Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, 
Dk. Shukuru Kawambwa na kulia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Profesa Samwel Wangwe.
Waziri wa Elimu na Mafunzoya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (kulia) na Mama Maria Nyerere (kushoto), wakizindua ujenzi wa Jengo Kuu la Elimu la Chuo Kikuu Huria Tanzania. 
Mwakilishi kutoka Ubalozi wa Ufaransa, Francois Leonardi, akisalimiana na Mama Maria Nyerere (wa kwanza kushoto), Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Profesa Samwel Wangwe (watatu kulia), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (katikati) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly Mbwette. 
Waziri wa Elimu na Mafunzoya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto), akizungumza jambo na viongozi wa Chuo hicho, mara baada ya kumalizika uzinduzi huo leo.
Mama Maria Nyerere pamoja na Waziri wa Elimu na Mafunzoya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa (katikati), wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu Huria, mara baada ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo hilo leo. (Picha zote na Philemon Solomon wa Fullshangwe)

No comments:

Post a Comment