TANGAZO


Wednesday, September 5, 2012

Makamu wa Rais, Dk. Bilal afungua Mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), mjini Zanzibar, kujadili uhalifu wa Kimataifa

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Generali, Said Mwema, wakati alipofika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo, Sept 05 kwa ajili ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi. (Picha zote na OMR)
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, kutoka nchi mbalimbali za Kusini mwa Afrika (SADC), wakiwa katika mkutano huo, uliofanyika leo Sept 05, 2012, ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo, kutoka Zambia wakiwa kwenye mkutano huo, wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa. Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wamekutana leo Sept 05, 2012, ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar, kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (katikati), akijumuika kuimba wimbo wa Taifa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Generali, Said Mwema (wa pili kushoto), wakati alipofika ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo Sept 05, 2012 kwa ajili ya kufungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi.
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Generali, Said Mwema, akisoma hotuba yake ya ukaribisho wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi za Afrika kiulinzi. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Plisi, Inspekta Genarali, Saidi Mwema, baada ya kuufungua mkutano wa Wakuu wa Majeshi ya Polisi kutoka Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), wa kujadili uhalifu wa Kimataifa kuhusu madawa ya kulevya na kuimarisha uhusiano kwa nchi zaAfrika kiulinzi. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Afrika ya Kusini.
Picha ya pamoja ya Wakuu hao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal, mara baada ya Makamu wa Rais kuufungua mkutano wao huo leo, Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar. (Picha zote na OMR)

No comments:

Post a Comment