![]() |
Mufti Sheikh Issa Shaaban Bin Simba |
Na Joseph Mwambije,
Songea
SHEIKH Mkuu wa Wailsamu nchini, Mufti Issa Shabaan bin Simba amewata Waislamu ambao wanahitaji kujua idadi yao, kujihesabu wenyewe kwenye Misikiti yao badala ya kuzuia zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa kugoma kuhesabiwa na kuzuia wengine kuhesabiwa.
Alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza kwenye Baraza la Idd Elftri lilofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Songea ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha Ibada ya Idd Eftri iliyofanyika Kitaifa Mkoani Ruvuma.
Kiongozi huyo wa Waislamu Nchini amwataka Waumini wa dini hiyo kuachana na baadhi ya Viongozi wa Kiislamu wanaowahamasisha kuiasi Serikali kwa kuchochea vurugu kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha miongozo ya Kurani tukufu inayowataka kutii mamlaka ilimradi isiende tofauti na Mungu.
‘Waislamu wajihesabu wenyewe misikitini wasiitegemee Serikali kuwatolea hesabu yao kwamba wako wangapi hivyo basi kupinga Zoezi la Sensa kwa madai ya kutokuwepo kipengele kinachoeleza dini si sahihi’alisema Mufti Simba.
Aliwataka kuwa na Kompyuta katika Misikiti yao na kuhifadhi kumbukumbu zao na kujua wana vijana,watoto na yatima wangapi badala ya kupinga kuhesabiwa kwa maendeleo ya Nchi.
Sheikh Simba alifafanua kuwa Sensa ya watu na makazi ni kwa maendeleo ya
Nchi hivyo kupinga si sahihi na na kuwataka Waumini wa Kiislamu kutopinga maendeleo na kuwapuuza Masheikh wanawahamasisha kupinga maendeleo.
Katika hatua nyingine amewataka Waislamu kutenda mema ili kuongeza idadi yao na kubainisha kuwa licha ya uchache wao watang’ara ikiwa watajizuia kutenda maovu.
‘Mjizuie kutenda maovu kwa kuwa Mwanadamu asiyejizuia kutenda maovu mwisho wake daima huwa ni mbaya na msipokuwa na uwezo wa kujizuia kutenda maovu ibada ya funga kwenu haina maana’alisema na kufafanua
Katika kipindi chote cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani mmejizuia kutenda maovu muendelee hivyo na kuendeleza kazi mliyopewa na Mungu ya kutenda mema hivyo Muwe viumbe mliozaliwa upya baada ya Mfungo.
Amewataka Waislamu kuachana na maneno ya kwamba wao wanaonewa na badala yake wawe wanachanga pesa kwa ajili ya kuwasaidia yatima na wajane na kwa maendeleo kwa ujumla huku wakikataza maovu na kuhimiza mema.
Akizungumza kwenye Braza hilo Katibu wa Baraza la waislamu Tanzania(BAKWATA) Mkoa wa Ruvuma Sheikh Abdul Shakhil alisema wana mpango wa kujenga Kituo cha Afya na Sekondari katika Manispaa ya Sengea.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu ambaye alimwakilisha Rais Kikwete ambaye alitakiwa kuwa Mgeni Rasmi alisema katika kipindi cha hivi karibuni umezuka utamaduni mgeni kwa Watanzania wa kuchochea chuki na uhasama miongoni mwa Watanzania na kuwataka Viongozi wa dini kukemea vitendo hivyo.
Alisema kuwa gharama ya machafuko ni kubwa sana kwa Taifa hivyo aliwataka Watanzania kutofurahia vitendo vya kuchochea machafuko na badala yake kuendelea kuitunza tunu ya amani,umoja wa Kitaifa na mshikamano
Alisema Serikalikali itaendelea kushirikiana na Viongozi wa dini kwa kuwa inatambua,kuheshimu na kuthamini sana mchango wa dini katika mafanikio na maendeleo ya Taifa.
No comments:
Post a Comment