Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akibadilishana mawazo na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, kwenye viwanja vya hoteli ya Bwawani walipokutana kwa ajili ya Baraza la Eid El Fitri jana tarehe 19/08/2012.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barazala Mapinduzi, Dk. Ali Mohd Shein, akiwa pamoja na viongozi wakuu wa Zanzibar na viongozi wengine kwenye viwanja vya hoteli ya Bwawani wakati wa sherehe za Baraza la Eid El Fitri.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Amani Abeid Karume, kila mmoja akiwa na shauku ya kutaka kumweleza mwenzake chochote, walipokutana katika hoteli ya Bwawani kwa ajili ya Baraza la Eid El Fitri. Viongozi hawa ndio walioasisi maridhiano ya kisiasa Zanzibar na kupatikana Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbalimbali katika viwanjavya hoteli ya Bwawani, walipokutana kwa ajili ya Baraza la Eid El Fitri jana tarehe 19/08/2012. (Picha na Salmin Said - Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar)
No comments:
Post a Comment