TANGAZO


Monday, August 20, 2012

Rashid Matumla apigwa kwa ponti na Maneno Oswald




Bondia Maneno Oswald akitangazwa kuwa mshindi wa pambano hilo baada ya kumdunda Rashid Matumla kwa pointi.
Bondia Rashidi Matumla kushoto akioneshana umwamba wa kutupa masumbwi na Maneno Osward wakati wa mpambano wao uliofanyika usiku wa kuamkia leo, ukumbi wa Dar live Maneno alishinda kwa point. 
Maneno Oswald akimbana Rashid Matumla kwenye kona, wakati wa mpambano huo.
Bondia Maeno Oswald akijaribu kujinasua kwa Rashid Matumla, ambapo mabondia hao walipambana sambamba hadi hatua ya mwisho ya pambano hilo.
MPAMBANO wa ndondi baina ya mabondia Maneno Oswald na Rashid Matumla ambao ulifanyika ukumbi wa maraha wa Dar Live Mbagala, jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, katika kuadhimisha Sikukuu ya Idi el Fitr, ulishuhudia Oswald akimchakaza Matumla kwa pointi.
Mbali na mpambano huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo, kulikuwa pia na burudani za aina mbalimbali, likiwemo disko la watoto ambao pia walifurahia kuogelea katika bwawa maalum na michezo mingine mingi. Kwa upande wa muziki kulikuwa na shoo kali zilizofanywa na wanamuziki Juma Nature, Mwasiti Almasi, Estelinah Sanga ‘Linah’, Maunda Zorro na kundi zima la Jahazi Modern Taarab, likiongozwa na mfalme, Mzee Yusuf. (Picha: Musa Mateja na Richard Bukos/GPL)
Matumla na Maneno wakisulubiana jukwaani wakati wa mpambano huo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Juma Kassim ‘Juma Nature’, akiofanya vitu vyake kwenye ukumbi huo, wakati wa pambano hilo.
Kiongozi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf akiwapagawisha mashabiki wake. 
Mwasiti Almasi akikamua na wacheza shoo wake.
Maunda Zorro akionesha umahiri wake wa kuimba na kuzirudi ngoma kwenye jukwaa.
Sadick Momba (kushoto), akipambana na Venance Mponji katika mpambano wa utangulizi kabla ya Matumla na Maneno hawajatwangana, ambapo Sadick aliibuka mshindi kwa kumtwanga Mponji.
Julius Thomas (kushoto), akizidunda na Jumanne Kirumbe kabla ya Maneno Oswald na Matumla kupanda ulingoni. Julius alishinda mpambano huo.
Mmoja wa wasanii wa kundi la Mabaga Fresh, ambaye sasa yuko katika kundi la Wanaume Halisi, JB Mkuu wa Maadui akitumbuiza kwenye jukwa hilo.
Mwimbaji wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Khadija Yusuf akiimba wakati kundi hilo lilipokuwa likitumbiza jukwaani hapo.
Malkia wa Bendi ya Jahazi Modern Taarab, Leila Rashid akiimba wakati wa pambano la Matumla na Maneno kwenye ukumbi huo wa Dar Live, Mbagala Zakhem.
Watoto wakicheza muziki ndani ya bwawa la kuogelea.
Baadhi ya umati uliokuwa ndani ya ukumbi huo, ukifuatilia burudani na mapambano ya ngumi yaliyokuwa yakifanyika ukumbini humo.

No comments:

Post a Comment