Oscar Joshua wa Yanga (kulia), akikimbiza mpira na Semmy Kessy wa African Lyon wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Taifa, Dar es salaam leo jioni kwa ajili ya maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom nchini. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
David Luhende wa Yanga, akimtoka Johanes Kajuna wa African Lyon katika mchezo huo.
Mashabiki wa Yanga, wakifuatilia mchezo huo, wakati timu hizo zilipokuwa zikimenyana uwanjani hapo leo jioni.
Wachezaji wa Yanga wakimpongeza Simon Msuva (kulia), baada ya kufunga bao la tatu la timu hiyo dhidi ya African Lyon katika pambano hilo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Zuberi Ubwa wa African Lyon (kulia), akikokota mpira huku akifuatwa na Jerryson Tegete wa Yanga wakati wa mchezo huo.
Musasa Obina wa African Lyon (kushoto), akipambana na Oscar Job wa Yanga.
Mpaka mwisho wa mchezo huo, matokeo ya mchezo huo, alikuwa kama yanavyoonekana kwenye ubao wa matokeo, Yanga SC 4 : African Lyon 0.
No comments:
Post a Comment