TANGAZO


Saturday, August 18, 2012

Vijana wa Simba waichanachana Mtibwa Sugar, Uwanja wa Taifa

 Wachezaji wa Simba na Mtibwa Sugar, wakiingia uwanjani tayari kwa mpambano wao wa ubingwa wa mashindano ya BancABC 2012, Sup8r 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

Waziri wa achezaji wa Simba na Mtibwa Sugar, wakiingia uwanjani tayari kwa mpambano wao wa ubingwa wa mashindano ya ubingwa wa BancABC 2012, Sup8r 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala, akiikagua timu ya Simba kabla ya kupambana na Mtibwa Sugar, katika mpambano wao wa kuwania ubingwa wa mashindano ya BancABC 2012, Sup8r 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala, akitoa nasaha kwa wachezaji wa Simba na Mtibwa Sugar, mara baada ya kuzikagua timu hizo, tayari kwa mpambano wao wa ubingwa wa mashindano ya BancABC 2012, Sup8r 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Wachezaji wa Simba na Mtibwa Sugar, wakisalimiana mara baada ya kukaguliwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala, kabla ya mpambano wao wa fainali ya ubingwa wa BancABC 2012, Sup8r 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Kikosi cha timu ya Simba, kikipiga picha ya kumbukumbu kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa fainali ya michuano ya BancABC, Sup8er 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Kikosi cha timu ya Simba, wakipiga picha ya kumbukumbu kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa fainali ya michuano ya BancABC, Sup8er 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Kikosi cha timu ya Mtibwa Sugar, kikipiga picha ya kumbukumbu kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa fainali ya michuano ya BancABC, Sup8er 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Wachezaji Edward Christopher (kulia) na Rashid Ismail wa Simba, wakishagilia bao la kwanza la timu hiyo lililofungwa na Christopher dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa fainali ya michuano ya BancABC, Sup8er 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Wachezaji wa Simba, wakishagilia bao la kwanza la timu hiyo, lililofungwa na Edward Christopher (kulia), dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa fainali ya michuano ya BancABC, Sup8er 2012, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


 Edward Christopher wa Simba (kushoto), akitafuta mbinu ya kumtoka Yussuf Nguya wa Mtibwa Sugar wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

 Edward Christopher wa Simba (kushoto), akijaribu kumpiga chenga na kumtoka Yussuf Nguya wa Mtibwa Sugar, wakati wa mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

 Mashabiki na wanachama wa Simba wakifuatilia mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

 Mchezaji Rashid Ismail wa Simba (kulia), akimtoka Salum Swedi wa Mtibwa Sugar katika mchezo huo, uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo jioni na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 na kutwaa ubingwa wa mashindano hayo.

Rashid Ismail wa Simba (kulia), akimpelekesha Salum Swedi wa Mtibwa Sugar, wakati wa wa mchezo huo wa fainali, uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo jioni na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 4-3.

 Mchezaji Malika Ndeme wa Mtibwa Sugar, akijaribu kumzuia Ibrahim Rajab wa Simba katika mchezo huo.

 Hadi mwisho wa mchezo huo, uliochezwa kwa dakika 120, unamalizika Simba ilikuwa mabao 4 na Mtibwa Sugar 3 kama ubao wa matokeo unavyoonesha.

 Mashabiki na wanachama wa Simba wakifuatilia mchezo huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Wachezaji wa timu ya Vijana ya Simba, wakimbemba kocha wao, Suleiman Matola baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 4-3 katika mchezo wa fainali ya BancABC Sup8r 2012, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

Mmoja wa makocha wa timu ya Mtibwa, Patric Mwangata (aliyewahi kuwa golika wa Simba kushoto), akimpongeza Suleiman Matola kwa timu yake kufanikiwa kushinda katika mchezo huo.

Makocha wa timu ya vijana ya Simba, Suleiman Matola (kushoto), Amri Said (kulia), wakiwa na Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Godfrey Nyange 'Kaburu', wakipiga picha ya kumbukumbu na wachezahji wa timu hiyo, mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

 Baadhi ya waandishi na wadau wa mpira wa miguu, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka uwanjani humo.

 Mfungaji Bora, Edward Christopher wa Simba, aliyefunga mabo 8 katika michuano hiyo, akikabidhiwa mfano wa hundi ya kiasi cha shs. mil. 2, 000, 000 na Mkurugenzi Mkuu wa Fedha, Mwalimu Zubery, baada ya kuibuka kinara wa ufungaji mabao.


Waziri wa Habari Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala, akimkabidhi kombe la ubingwa wa mashindano ya BancABC Sup8r 2012, Nahodha wa timu ya vijana ya Simba, Hassan Hatibu, baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 4-3, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


Waziri wa Habari Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala, akimkabidhi kombe la ubingwa wa mashindano ya BancABC Sup8r 2012, Nahodha wa timu ya vijana ya Simba, Hassan Hatibu, akisaidiwa na Mwenyekiti wa timu hiyo, Ismail Rage, baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 4-3, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


Wachezaji wa timu ya Simba, wakifurahia kombe lao mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala (hayupo pichani), baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 4-3, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.


Wachezaji wa timu ya Simba, wakifurahia kombe lao la Ubingwa wa michuno ya BancABC Sup8r 2012, mara baada ya kukabidhiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenella Mukangala (hayupo pichani), baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 4-3, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment