TANGAZO


Sunday, August 19, 2012

Rais Shein ashiriki Swala, Baraza Idi na kuonana na Masheikh mjini Zanzibar

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa tano kushoto), akijumuika na Waislamu wengine, viongozi wa Serikali pamoja na wananchi  mbali mbali katika Sala ya Idi El Fitri iliyosaliwa Kitaifa katika Msikiti wa Mwembeshauri, Mjini Zanzibar leo. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein (wa tano kushoto), akiswali pamoja na Waislamu wengine, viongozi wa Serikali na wananchi  mbali mbali Swala ya Idi El Fitri iliyosaliwa Kitaifa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar jana. 

Baadhi wa waumini wa Dini ya Kiislamu, wakiwa katika  Sala ya Iddi el Fitri iliyosaliwa kitaifa katika msikiti wa Mwembesahauri, Mjini Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein,  akisalimiana na watoto walioshiriki katika Sala ya Iddi el Fitri, iliyowajumuisha waislamu kutoka mitaa mbalimbali ya Mji wa Zanzibar na kusaliwa Kitaifa katika Msikiti wa Mwembeshauri Mjini Zanzibar leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akiwashukuru mashekhe  katika ukumbi wa Ikulu, Mjini Zanzibar walipofika kusalimiana naye leo. Pia kumshukuru Mola kwa kuwawezesha kumaliza Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa salama na kusheherekea Sikukuu ya Idi el Fitri.

Mashekhe wakiitikia dua iliyokuwa ikiombwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, baada ya kusalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, walipofika Ikulu, Mjini Zanzibar leo katika kusheherekea Sikukuu ya Idi el Fitri.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akifuatana na wasaidizi  wake akielekea katika viwanja vya Ikulu, Mjini Zanzibar kutoa mkono wa Idi kwa watoto na wananchi waliofika katika viwanja hivyo leo, ikiwa ni katika 
kusheherekea Sikukuu ya Idi el Fitri.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akitoa mkono  Idi kwa watoto na wananchi waliofika katika viwanja vya Ikulu, Mjini Zanzibar leo, ikiwa ni katika kusheherekea Sikukuu ya Idi el Fitri.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akitoa mkono  Idi   kwa watoto na wananchi waliofika katika Viwanja vya Ikulu, Mjini Zanzibar leo, ikiwa ni katika kusheherekea Sikukuu ya Idi el Fitri.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea salamu ya heshima ya Gwaride Maalum la kikosi cha Polisi wa kuzuia ghasia (FFU), kabla ya kuanza kwa shughuli za Baraza la Idi el Fitri, lililofanyika leo katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.

Baadhi ya viongozi na wananchi wa Manispaa ya Mji wa Unguja, waliofika kaika ukumbi wa Salama Bwawani, Mjini Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiwahutubia wananchi katika Baraza la Idi el Fitri leo, katika shamra shamra za Sikukuu ya kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. 


Baadhi ya viongozi na wananchi wa Manispaa ya Mji wa Unguja, waliofika kaika ukumbi wa Salama Bwawani, Mjini Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiwahutubia wananchi katika Baraza la Idi el Fitri leo, katika shamra shamra za Sikukuu ya kumalizika kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. 


Baadhi ya Mabalozi wa nchi mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiwahutubia wananchi katika Baraza la Eid el Fitri, lililofanyika leo katika ukumbi wa Salama Bwawani, Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akiwatubia wananchi katika sherehe za Baraza la Iddi el Fitri lililofanyika leo ukumbi wa Salama Bwawani Hotel, Mjini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, akiwatubia wananchi katika sherehe za Baraza la Iddi el Fitri lililofanyika leo, katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Zanzibar.

Shein ahimiza wananchi kushiriki zoezi la Sensa

Na Rajab Mkasaba, 

Ikulu Zanzibar. Zanzibar                                                                                               

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein, amewataka wananchi kutowapa nafasi wasioitakia mema Zanzibar na badala yake wawajibike katika kufanikisha zoezi la sensa ambalo ni muhimu katika maendeleo nchini.

Alhaj Dk. Shein aliyasema hayo leo, katika hotuba yake aliyoitoa katika Baraza la Idd El Fitri huko katika hoteli ya Bwawani mjini Unguja.

Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa inasikitisha kuwepo kwa baadhi ya watu wanaowashawishi wenzao wasikubali kuhesabiwa kwa visingizio visivyokuwa na msingi.

Alisema kuwa mafundisho ya dini zote hayapingi suala la kuhesabiwa kwa nia ya kupanga na kuleta maendeleo ya mwananchi na nchi yake.

“Tunakumbuka kuwa nchi yetu imeshafanya zoezi la sensa kwa vipindi mbali mbali huko nyuma kwa ufanisi mkubwa  bila ya kuwepo kisingizio chochote katika suala hili”,alisema Alhaj Dk. Shein.

Aidha, Alhaj Dk. Shein alisema kuwa katika siku za hivi karibuni, Zanzibar ilikabiliwa na viashirio vya kuvunjika kwa amani, utulivu na mshikamano na kusisitiza kuwa kuvuruga kwa amani ni jambo la muda mfupi lakini kuirudisha inachukua muda mrefu.

Alisema kuwa katika kipindi hicho yameshuhudiwa matukio mawili makubwa likiwemo lile la tarehe 26, 27 na 28 Mei na la 20 Julai mwaka huu matukio ambayo yameitia doa jamii ya Zanzibar ambayo imejijengea sifa nzuri pamoja na amani na utulivu.

Alhaj Dk. Shein alisema kuwa kuvunjia kwa amani husababisha athari ya vitu na watu wasio na hatia na kutoa wito kwa wananchi wote kuepuka vitendo vya uvunjaji wa amani na vinavyopelekea kuathiri watu na mali zao.

Alieleza kuwa inapaswa kujua kuwa vitendo kama hivyo vinaathiri sana jitihada za nchi katika shughuli za maendeleo na ukuaji wa uchumi hasa katika kuimarisha sekta ya utalii ambayo Serikali imeamua kuiimarisha kwa kauli mbiu’Utalii kwa wote’.

Dk. Shein aliyitumia futrsa hiyo kuwatanabahisha wanaopanga na kushabikia vitendo vya uvunjaji sheria, amani na utulivu kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa itaendelea kuchukua hatua za kisheria kwa wanaosababisha vurugu na kukiuka taratibu za sheria.

Hata hivyo aliwasihi wananchi kutojiingiza kwenye vitendo vinavyopelekea kuvunjia kwa amani na badala yake wafanye mambo ya uadilifu yanayozingatia sheria zilizopo na maadili yake ‘Tutumie busara katika kuyatatua matatizo yetu yanapotokea, kwa njia ya mazungumzo kwani hii ndio njia pekee... hakuna lisilozungumzika”,alisisitiza Dk. Shein.

Alisisitiza kwua Serikali ina wajibu wa kulinda haki na uhuru wa wananchi wake na mali zao ambapo pia, Dk. Shein alilipongeza Jeshi la Polisi kwa mara nyengine tena kwa kazi nzuri walioifanya ya kutuliza fujo zilizotokea.

Akieleza mafanikio yaliopatikana kwa kipindi kifupi tangu muundo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya Umoja wa Kitaifa ulipoanza, Zanzibar imeweza kupiga hatua kubwa katika nyanja mbali mbali za kijamii na kiuchumi.

Alisema kuwa mafanikio hayo yamepatikana kutokana na viongozi na wananchi kuishi kwa mashirikiana na kuvumiliana kisiasa ambapo kwa upande wa Serikali, viongozi wamekuwa na ushirikiano wa karibu na kuweza kufanya kazi kwa misingi ya Katiba, sheria na kuheshimiana kwa manufaa ya nchi.

Akizungumzia  kuzama kwa meli ya MV Skagit, Dk. Shein alisema kuwa aliwataka wananchi kwuasaidia ipasavyo na kumuomba Mola awalaze peponi wote waliopoteza maisha katika msiba huo na kueleza kuwa Serikali imechukua hatua mbali mbali kuhusu maafa hayo.

Katika kupunguza tatizo la usafiri wa baharini alieleza kuwa tayari ameshaipa maagizo Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo  kuhakikisha kwamba katika kipindi cha miezi miwili ijayo wanakamilisha taratibu za kuagiza meli mpya kubwa  kwa ajili ya abiria na mizigo.

Alisema kuwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu katika kipindi cha miezi 15 ijayo inatarajiwa  meli hiyo kufika nchini, meli ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,000 na mizigo tani 200. Pamoja na hayo, Dk. Shein  aliwasisitiza wananchi kuendeleza mafunzo waliyoyapata katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mapema asubuhi Dk. Shein aliungana na viongozi mbali mbali pamoja na wananchi katika sala ya Idd el Fitri huko katika msikiti wa Mwembeshauri mjini Unguja na baada ya hapo alifika Ikulu mjini Zanzibar na kusalimiana na baadhi ya Masheikh, Makadhi na viongozi wengine wa dini na serikali.

No comments:

Post a Comment