Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Meatu alipotembelea pori la akiba la Maswa. Nyuma yake ni Mbunge wa Jimbo la Kisesa Mkoa wa Simiyu.

Mkuu wa Wilaya ya Meatu, Rosemary Kirigini akitoa taarifa ya maendeleo ya pori la akiba Maswa kwa Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu aliyetembelea pori hilo leo.

Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Wilaya ya Meatu, Mpina akitoa salamu zake kwa wafanyakazi na viongozi wa pori la akiba Maswa.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa pori la akiba Maswa.

Naibu Waziri wa Maliasli na Utalii, Lazaro Nyalandu (kushoto), akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mkoa wa Simiyu, Mpina muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa pori la akiba la Maswa.

Baadhi ya viongozi waliofuatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwenye boti kwenda kukagua maendeleo ya hifadhi ya kisiwa cha Saanane.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (kulia), akiwa kwenye boti akielekea kukagua hifadhi ya kisiwa cha Saanane jijini Mwanza.

Mwandishi wa habari wa MO BLOG, Nathaniel Limu muda mfupi baada ya kuteremka uwanja wa ndege wa jijini Mwanza kutoka kwenye ndege iliyokuwa imembeba Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu, aliyekuwa katika ziara hiyo. (Picha na mdau wetu)