TANGAZO


Wednesday, August 8, 2012

Kampuni ya Steps, Wasanii wakamata wezi wa kazi zao jijini Dar es Salaam

 
Baadhi ya wasanii pamoja na askari Polis wakiwa wamelizingira duka lililokuwa linauza kazi za wasanii feki

 Baadhi ya mizigo ya DVD mpya ambazo ni feki, zkiwa zimekamatwa leo jijini Dar es Salaam. 
 Msanii wa filamu nchini, Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto na Jacob Stevin 'JB' wakiwa katika duka ambalo lilikuwa linauza kazi zao, ambazo zilikuwa ni feki, ambapo walikamatwa kwa kushirikiana na Kampuni ya usambazaji ya Steps Entantainment ya jijini Dar es Salaam jana.
 Msanii wa muziki wa tarab, Mzee Yussuf (kushoto), akiangalia moja ya kazi zake  iliyokuwa feki, zilizokamatwa na wasanii wenyewe kwa kushirikiana na Kampuni ya Steps Entertainmet ya jijini  Dar es Salaam leo.
 Msanii Mohamed Nice 'Mtunisi' akizungumza na waandishi wa habari, kuelezea jinsi walivyokamata mzigo feki wa kazi za wasanii mbalimbali kwa kushirikiana na Kampuni ya steps Entertainment ya jijini, inayosambaza kazi za wasanii.
 Baadhi ya wananchi wakiwa wamezagaa kushuhudia ukamatwaji wa kazi feki za wasanii makutano ya mitaa wa Magila na Likoma, Kariakoo jijini Dar es salaam leo.
 Moja ya gari lililokuwa limejaa kazi feki za wasanii mbalimbali nchini zinazouzwa baada ya kurudufiwa kinyume cha sheria na kukosesha wasanii mapato mazuri.
 Msanii Kapteni Rado, akikagua kazi zake mpya ambapo kazi yake mpya ijulikanayo kama 'Hatiani' iliyoingia smtaani jana
imeshachakachuliwa na kuingizwa sokoni. 
Msanii nice akionesha kusikitishwa na wizi wa kazi zao na watu wasio waaminifu, wanaojitafutia riziki kwa kutumia migongo ya wenzao.
Msanii Mohamed Nice, akilia kwa uchungu baada ya kukuta kazi zao zilizokuwa zikuzwa katika moja ya duka kwenye mtaa wa Magila na Likoma, jijini Dar es salaam leo.

Mmoja wa watuhumiwa wa kurudufu kazi za wasanii akihojiwa na waandishi wa habari, akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi. (Picha zote na mpiga picha wetu)

No comments:

Post a Comment