TANGAZO


Wednesday, August 8, 2012

Benki ya KCB Tanzania yatoa msaada Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar

 Katibu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Omar Abdallah akipokea msaada wa vyandarua pamoja na mashine ya kumsaidia mgonjwa kupumulia (Oxygen Contentrator), vyenye thamani ya milioni tano kwa niaba ya Hospitali ya Mwembeladu kutoka kwa Meneja wa banki ya KCB tawi la Stone Town, mjini Zanzibar, Rajabu Ramia. Kulia ni Meneja wa Biashara wa benki ya KCB Zanzibar, Abdallah Mshangama.

 Katibu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Omar Abdallah (kushoto), akipokea mashine ya kupumlia wagonjwa (Oxygen Contentrator), kwa niaba ya Hospitali ya Mwembeladu kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar, Said Amour (katikati), Meneja wa banki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar, Rajabu Ramia. Benki hiyo ilitoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tano.

 Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar, Rajabu Ramia, akimkabidhi Muuguzi msaidizi wa Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar, Zawadi Suleiman msaada wa vyandarua pamoja na mashuka 50 na vifaa mbalimbali vyenye thamani ya jumla ya Shilingi milioni Tano.
 Ofisa Mahusiano wa Benki ya KCB Tanzania, Martha Edward akimpatia zawadi ya tende Amina Ahamed, alielazwa katika wodi ya wazazi kwenye Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar mara baada ya wafanyakazi wa Benki ya KCB, kufika katika Hospitali hiyo kwa lengo la kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye jumla ya thamani ya Shilingi milioni tano.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya KCB, tawi la Zanzibar, wakiwa kwenye picha ya pamoja na wauguzi wa Hospitali ya Mwembeladu mjini Zanzibar mara baada ya wafanyakazi wa Benki hiyo, kufika katika hospitali hiyo kwa lengo la kutoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye jumla ya thamani ya Shilingi milioni tano.

No comments:

Post a Comment