Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi kombe, Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma Salum Ally, baada ya Halmashauri ya Wilaya hiyo, kuwa mshindi wa jumla katika maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima 'Nanenane', yaliyomalizika leo, Agosti 8, 2012, wakati alipokuwa akiyafunga maonesho hayo, Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mmoja kati ya wajasiriamali wa vikundi vya wakulima, wakati alipokuwa akiyafunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nanenane yaliyomalizika leo, Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipowasili kwenye Viwanja vya Nzuguni, mjini Dodoma leo, Agosti 8, 2012 kwa ajili ya kuyafunga rasmi maonesho hayo.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete, kufunga rasmi maonesho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nanenane yaliyomalizika leo, Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akionesha tuzo aliyokabidhiwa kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Rais katika kusimamia na kuendeleza Kilimo Kwanza, wakati Makamu alipokuwa akiyafunga rasmi maonesho ya Sikukuu ya Wakulima ya Nanenane, Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo Agosti 8, 2012. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza.
Makamu wa Rais, Gharib Bilal, akimkabidhi kombe mmoja wa washiriki katika maonesho ya Siku ya Wakulima, Nanenane, wakati akiyafunga maonesho hayo leo.
No comments:
Post a Comment