Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, akizungumza baada ya kumalizika mashindao ya kusoma na kuhifadhi Kur'an kwa nchi za Afrika ya Mashariki, ukumbi wa PTA, Sabasaba Kilwa Road, Dar es Salaam leo kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.
Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwa na Mlezi wa taasisi ya Al Hikma Education Centre, iliyoandaa mashindano hayo, Sheikh Abdulkadir Mohamed, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka kwenye mashindano hayo, ukumbini humo leo.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria kwenye mashindano hayo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye mashindano hayo, ukumbini humo leo.
Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi na Mlezi wa taasisi ya Al Hikma Education Centre, iliyoandaa mashindano hayo, Sheikh Abdulkadir Mohamed, wakimpongeza mshindi wa kwanza kwa waliohifadhi juzuu 3, Shamsia Shaaban, wakati akimkabidhi zawadi ya Radio na fedha taslim pamoja na cheti. Kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim.
Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti na fedha taslim, mshindi wa 3 katika kuhifadhi Kur'an juzuu 7, Abdulbasti Sultan, wakati wa fainali za mashindano ya kusoma na kuhifadhi Kur'an yaliyotayarishwa na taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim na katikati ni Mlezi wa taasisi hiyo, Sheikh Abdulkadir Mohamed.
Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti na fedha taslim, mshindi wa pili katika kuhifadhi Kur'an juzuu 10, Ashura Amani wa Almadrasatu Ass-habu Lkahafu ya Yombo Temeke, wakati wa fainali za mashindano ya kusoma na kuhifadhi Kur'an yaliyotayarishwa na taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam. Kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim na katikati ni Mlezi wa taasisi hiyo, Sheikh Abdulkadir Mohamed.
Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti na fedha taslim, mshindi wa kwanza katika kuhifadhi Kur'an juzuu 10, Seif Salim, ambaye ni mlemavu wa macho (kipofu), kutoka madrasatu Aljadida ya Wete - Pemba, wakati wa fainali za mashindano ya kusoma na kuhifadhi Kur'an yaliyotayarishwa na taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mlezi wa taasisi hiyo, Sheikh Abdulkadir Mohamed.
Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akimkabidhi cheti, bodaboda na fedha taslim, mshindi wa 3 katika kuhifadhi Kur'an juzuu 30, Adam Seif wa madrasatu El Hikma ya Temeke jijini Dar es Salaa, wakati wa fainali za mashindano ya kusoma na kuhifadhi Kur'an yaliyotayarishwa na taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mlezi wa taasisi hiyo, Sheikh Abdulkadir Mohamed na kulia ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim.
Mshindi wa 3 katika kuhifadhi Kur'an juzuu 30, Adam Seif wa madrasatu El Hikma ya Temeke jijini Dar es Salaa, akipanda bodaboda yake baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi katika fainali za mashindano ya kusoma na kuhifadhi Kur'an yaliyotayarishwa na taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam leo viwanja vya Sabasaba, Kilwa Road.
Mshindi wa Pili wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Kur'an, yaliyoandaliwa na taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam, Abdallah Said Ali kutoka Pemba, akiiangalia zawadi yake ya Bajaj baada ya kukabidhiwa na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (kushoto), Dar es Salaam leo. Katikati ni Mlezi wa taasisi hiyo, Sheikh Abdulkadir Mohamed.
Mshindi wa Pili wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi Kur'an, yaliyoandaliwa na taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam, Abdallah Said Ali kutoka Pemba, akikabidhiwa funguo ya Bajaj yake, aliyoshinda katika kusoma na kuhifadhi Kur'an, ukumbi wa PTA, Sabasaba jijini Dar es Salaam leo na mmoja wa wageni wa mashindano hayo, Shekh Hussein Ahmad Badani. Katikati ni mgeni Rasmi, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi.
Mshindi wa Kwanza wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi kwa nchi za Afrika ya Mashariki, yaliyoandaliwa na taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam, Abdulrrahaman Ramadhan wa Dodoma, akikabidhiwa zawadi zake za komputa ndogo, msahafu maalum wa Kur'an na dola za Marekani 4, 000 na mgeni rasmi, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, Dar es Salaam leo.
Mshindi wa Kwanza wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi kwa nchi za Afrika ya Mashariki, yaliyoandaliwa na taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam, Abdulrrahaman Ramadhan wa Dodoma, akikabidhiwa zawadi ya msahafu maalum wa Kur'an na dola za Marekani 4, 000 na mgeni rasmi, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati), akisaidiana na mmoja wa wageni waalikwa, Sheikh Hussein Badani (kushoto), Dar es Salaam leo.
Mshindi wa Kwanza wa mashindano ya kusoma na kuhifadhi kwa nchi za Afrika ya Mashariki, yaliyoandaliwa na taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam, Abdulrrahaman Ramadhan, akikabidhiwa zawadi ya komputa ndogo, msahafu maalum wa Kur'an na dola za Marekani 4,000 na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (katikati), Dar es Salaam leo. Kushoto ni mmoja wa wageni waalikwa, Sheikh Hussein Badani.
Baadhi ya Maulamaa wa Kiislamu waliokuwepo katika hafla hiyo, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka ukumbini hapo.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakitendeka katika hafla hiyo, ukumbini hapo leo.
Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto), akiitikia dua na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salim (kulia), Mlezi wa taasisi ya Al Hikma Education Centre ya jijini Dar es Salaam, Sheikh Abdulkadir Mohamed, waandaaji wa mashindano hayo, iliyokuwa ikisomwa na mmoja wa wageni wa mashindano hayo, Shekh Hussein Ahmad Badani (kushoto), mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.
Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (aliyemshika kichwa mmoja wa washindi wa mashindano hayo), akipiga picha ya kumbukumbu na washindi hao, mara baada ya kuwakabidhi zawadi zao.
Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kulia waliosimama) akipiga picha ya kumbukumbu na majaji wa mashindano hayo, mara baada ya kumaliza kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo jijini leo.
Mgeni rasmi Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, akifanya mahojiano na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza kukabidhi zawadi kwa washindi wa mashindano hayo jijini leo.
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea kwenye mashindano hayo, ukumbini hapo.
Baadhi ya waumini wanawake wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria kwenye mashindano hayo, wakiongozwa na Mlezi wa akina mama wa Bakwata, Bi. Fatuma Sururu (wa pili kushoto, mstari wa mbele), wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye mashindano hayo, ukumbini hapo leo.
No comments:
Post a Comment