Mama Maria Nyerere akabidhi matrekta wakulima wa Kwadelo Kondoa
Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nyerere akimkabidhi funguo za trekta moja kati ya kumi aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao, Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni Sheikh wa Kata ya Kwadelo.
Mkazi wa kijiji cha Kwadelo, Maulid Msema akipokea funguo moja kati ya 10 za matrekta yaliyokabidhiwa na Mama Maria Nyerere kwa ajili ya wakulima wa kijiji hicho, kilichopo wilayani Kondoa, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo kijijini hapo, katika hafla iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto anayeshuhudia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati.
Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati, akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Maria Nyerere kama shukurani ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.
Halafu akamkabidhi mkoba wa safari, kama akitaka kwenda Butiama
Kariati akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere wakati wa hafla hiyo.
Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Maria Nyerere, akimkaribisha, Diwani wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya Kondoa, Mkoa wa Dodoma, Alhaj Omar Kariati, wakati diwani huyo na ujumbe wake wa wakulima kumi, walipofika nyumbani kwa Mama Nyerere kwa ajili ya kukabidhiwa matrekta kumi kwa wakulima hao, katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa Mama Maria Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam jana (Picha zote na mdau wetu).
No comments:
Post a Comment