Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji akila kiapo cha utii kuashiria kuanza kazi rasmi ya kuitumikia klabu hiyo, baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi mdogo uliofanyika hivi karibuni. Kushoto ni Mzee wa Yanga, Jabir Katundu.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga akila kiapo.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Aaron Nyanda akila kiapo mbele ya mzee wa Yanga, Jabir Katundu.
Mjumbe wa bodi ya udhamini ya Yanga, Mama Fatuma Karume, akiteta jambo na viongozi wa Yanga.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji akiteta jambo na Makamu wake, Clement Sanga mara baada ya kula kiapo klabuni hapo.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji akimsikiliza Makamu wake, Clement Sanga mara baada ya kula kiapo klabuni hapo leo. |
Viongozi wa Yanga wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi ya udhamini ya klabu hiyo.
Mjumbe wa Bodi ya udhamini wa Yanga, Mama Fatma Karume, akiwa katika picha ya pamoja na wanacha wanawake wa Yanga.
Mjumbe wa Bodi ya udhamini wa klabu ya Yanga, Mama Fatma Karume akiwapungia mashabiki wa Yanga kabla ya kuanza kwa zoezi la kuwaapisha viongozi waliochaguliwa hivi karibuni. Kushoto ni mzee Jabir Katundu.
No comments:
Post a Comment