TANGAZO


Sunday, August 5, 2012

Januari Makamba aongoza mkutano wa Wanabumbuli jijini Dar es Salaam

Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba akiongea na wakazi kutoka wilaya ya  Lushoto, Jimbo la Bumbuli katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo, katika mkutano uliokuwa  unajadili maendeleo ya jimbo la  Bumbuli na kutambulisha shirika la maendeleo la  Bumbuli. January Makamba amesema katika kipindi cha mwaka 2011-2012, kiwango cha elimu ya Wilaya hiyo, kimekuwa chini na kusababisha vijana wengi katika mkoa wa Tanga kuwa na sifa ya kuuza chipsi na kubeba mizigo badala ya kufanya kazi kwenye makampuni.
Mkurugenzi wa Shirika la Bumbuli, Najim Msenga (kushoto), Mwenyekiti mteule wa Wilaya ya Bumbuli, Amiri Sheiza (kulia) na Katibu wa CCM, Wilaya ya Lushoto, Loth Ole Lemeirut (katikati), wakijadili jambo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo leo.

Wakazi kutoka Jimbo la Bumbuli, wakiwa katika mkutano huo, wa kujadili maendeleo ya Wilaya ya Bumbuli.

Kikundi cha ngoma kijulikanacho kwa jina la Mount Usambara Voice, kikitoa burudani katika mkutano huo.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi, Wilaya ya Lushoto, Loth Ole Lemeirut (kushoto) na mwanakamati wa Shirika la Bumbuli, Naaman Shauri, wakifuatilia kwa makini mada iliokuwa ikendelea katika mkutato huo leo. (Picha zote na mdau wetu)

No comments:

Post a Comment