TANGAZO


Friday, August 3, 2012

Mtoto aokotwa PPF Tower, alazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam


Mtoto ameokotwa eneo la PPF Tower, Jijini Dar es Salaam, saa sita mchana wa leo. Amekutwa amelala chini eneo hilo.
Ameletwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Askari wa Central Police. Mtoto huyu anakadiriwa kuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu hivi, kwa hiyo hawezi kuongea.

Yeyote anayemfahamu mtoto huyu au wazazi wa mtoto huyu, ajitokeze na kutoa taarifa sahihi kwetu kupitia namba yangu 0755 64 86 36 au 0715 64 86 36.

Mtoto tunaye Hospitalini, anaendelea kuhudumiwa. Tafadhali sambaza habari hii.

Imetolewa na;
Aminiel Buberwa Aligaesha
Afisa Uhusiano Mwandamizi
Hospitali ya Taifa Muhimbili




No comments:

Post a Comment