TANGAZO


Friday, August 3, 2012

Wizara ya Fedha ndani ya Maonesho ya Nane Nane mjini Dodoma

Kaimu Ofisa Uhusiano wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF), Hawa Kikeke (kushoto) na Ofisa Malipo wa Mfuko huo, Andrew Dayson (wa pili kushoto), wakiwasaidia  Maofisa wa Polisi juu ya kupata taarifa za michango yao mbalimbali, ambayo wamekwisha kuchangia tangu waingie katika utumishi wa umma wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya Wakulima ya Nane Nane leo, mjini Dodoma. (Picha zote na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dodoma)


Ofisa Uhusiano wa Chuo Mipango Dodoma, Sarah Mmari, akimwelimisha Yulis Otto, utaratibu wa kujiunga na masomo katika Chuo hicho, wakati mzee huyo, alioptembelea banda la Wizara ya Fedha leo katika maonesho ya Wakulima ya Nane nane, yanayoendelea mjini Dodoma.


Mwanasheria kutoka  Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana,  Emilia Mkubulo (kulia), akimwelimisha mmoja wa wananchi, faida za kununua hisa  leo, mjini Dodoma, alipotembelea banda la Wizara ya Fedha, kwenye maonesho ya Wakulima ya Nane nane.


Mtunza Kumbukumbu na Mhasibu, Abbas Mnyeto wa Wizara ya Fedha, wakiwasaidia wazee wastafu upande wa Kilimo, juu ya taratibu za kupata pesheni kwa watumishi wanapostaafu, leo mjini Dodoma walipokuwa kwenye banda la Wizara ya Fedha, kwenye maonesho ya Wakulima ya Nane nane.


Ofisa Uendeshaji wa Mfuko wa Pesheni kwa watumishi wa umma (PSPF), Kahenga Maulid (wa pili kulia) na Ofisa Malipo ya Pesheni wa Mfuko huo, Andrew Dayson (wa pili kushoto), wakiwasaidia watumishi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Monica Kung’aro (kushoto) na Mary Kulwijila (kulia), juu ya kupata taarifa za michango yao, mbalimbali ambayo wamekwisha kuchangia tangu waingie katika utumishi wa umma, wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya Wakulima ya Nane nane.




Ofisa Masoko kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), Said Mkomwa, akiwaelimisha wananchi, faida za kuwekeza katika mifuko iliyoanzishwa na Dhamana ya Uwekezaji Tanzania leo, mjini Dodoma walipotembelea banda la Wizara ya Fedha kwenye maonesho ya Wakulima ya Nane nane.

Ofisa kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Thabit Matotola (wa pili kushoto), akiwaelimisha wananchi leo, majukumu ya Wizara hiyo kwenye maonesho ya Wakulima Nane nane, mjini Dodoma. (Picha zote Maria wa HAZINA, Dodoma)


Ofisa Operesheni wa Mfuko wa Pesheni ya Watumishi wa Umma (PSPF), Kahenga Maulid (kushoto), akijibu maswali mbalimbali ya mwananchi huyo, aliyetaka kujua majukumu ya mfuko katika kumsaidia mtumishi wa umma, wakati wa maonesho ya Wakulima ya Nane nane, mjini Dodoma leo. 

Mchambuzi wa Masuala ya fedha kutoka Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana, Mariam Mtunguja, akimwelimisha mwamanchi, juu ya kazi na majukumu ya mamlaka hiyo, leo mjini Dodoama, wakati alipotembelea maonesho ya Wakulima ya Nane nane katika banda la Wizara ya Fedha.

Ofisa kutoka Dhamana ya Uwekezaji Tanzania(UTT), Mvumo Balati (kushoto), akiwaelimisha Polisi, faida ya kuwekeza katika mfuko huo, leo mjini Dodoma, wakati walitembelea maonesho ya Wakulima ya Nane nane, mjini Dodoma kwenye banda la Wizara ya Fedha.


Ofisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi wa Idara ya Kuondoa Umaskini, William Ghumbi (kushoto), akiwaelimisha wananchi juu ya MKUKUTA II, walipotembelea  banda la Wizara ya Fedha leo, mjini Dodoma kwenye maonyesho ya Wakulima ya Nane nane.

No comments:

Post a Comment