Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa |
Na Tiganya Vincent, Dodoma
MZEE mstaafu katika utumishi wa umma ameiomba Wizara ya Fedha kuongeza kiwango cha pesheni kinachotolewa kila mwezi kwa wastaafu kutoka elfu 50 kwa kima cha chini na kufikia nusu ya mshahara wa mtumishi wa cheo chake wakati anastaafu aliyekazini .
Hali hii itawasiadia wastaafu hao kujiona kuwa mchango wao waliotoa katika utumishi umma bado unathaminika katika utumishi wa umma.
Kauli hiyo imetolewa leo, mjini Dodoma na Ofisa Kilimo Mwandamizi Mstaafu Elias Sabuni alipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya Wakulima ya Nanenane, mjini Dodoma.
Sabuni alisema kuwa utaratibu wa kuongeza kwa watumishi waliokazini unapaswa pia kuwaangalia watumishi wastaafu kila Waziri wa Fedha anapowasilisha bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha unapofika.
Alisema kuwa gharama ya maisha inapanda na bei ya mahitaji muhimu katika masoko inaongezeka wakati fedha wanayopatiwa wastaafu haiongezeki kila mwaka wa fedha kitu kinachofanya maisha kwao kuwa magumu .
Sabuni alisema kuwa wakati watumishi waliopo kazini wanaongezewa kiwango cha mshahara ,wastaafu hawakumbuki wakati wa bajeti ya kila mwaka wa fedha na hivyo kukata tamaa.
Tukienda sokoni muuzaji hawezi kujua kuwa huyo ni mstaafu anapata kiasi kidogo cha fedha ukilinganisha na mwajiriwa aliyekazini ambaye anapata zaidi robotatu ya mstaafuîalisema Sabuni.
Ameomba Serikali iangalie upya ulipaji wa pesheni ya kila mwezi ili ikiwezekana wastaafu walipwe nusu ya mshahara wa watumishi waliokazini katika ngazi ya cheo chake cha mwisho wakati wa kustaafu.
Sabuni alisema kuwa hali hiyo itawasaidia kuondokana na ugumu wa maisha wanayokumbana nayo watumishi wanapostaafu.
Aliongeza kuwa kima cha chini cha sasa hivi ni shilingi elfu 50(50,000/-) ambacho hakiwezi kumsaidia mstaafu kumudu mahitaji muhimu ikiwemo gharama za kulipia umeme, huduma ya maji safi na taka, chakula na mahitaji mengine.
Hivyo , Sabuni ameoimba Serikali kuangalia upya Sheria inayohusu pesheni ili wastaafu wengi waweze kufurahia uzee wao na kuendelea kuchangia katika ujenzi wa Taifa.
Mzee sabuni alistaafu mwaka 1997 kama Afisa Kilimo Mwandamizi.
No comments:
Post a Comment