TANGAZO


Saturday, August 4, 2012

Maharamia washambulia meli za mafuta

Watu wenye silaha wameshambulia meli mbili nje ya eneo la mafuta la Nigeria, eneo la mdomo wa Mto Niger.
Pwani ya Niger Delta
Walinzi wawili waliuwawa na wawili kujeruhiwa.
Washambuliaji hao, ambao hawakujulikana, piya waliwateka nyara mabaharia wane.
Jeshi la wanamaji la Nigeria nalo linashiriki kuwasaka washambuliaji hao.
Shambulio hilo limetokea siku tu baada ya serikali ya Nigeria kutangaza kuwa itatumia satalaiti kuzuwia magendo ya mafuta katika eneo hilo, ambayo huuzwa kwenye soko la kimataifa.

No comments:

Post a Comment