TANGAZO


Saturday, August 11, 2012

Mkuu wa Mkoa, Meky Sadik azindua Shule ya Sekondari Maendeleo Madale jijini Dar es Salaam


 Mwenyekiti wa Kia Motors, Cho Kwi Hyun, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik mfano wa funguo ya moja ya magari manne ambayo kampuni hiyo imetoa kwa Shule ya Sekondari ya Maendeleo, iliyopo  Nakasangwe Madale jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla ya uzinduzi wa shule hiyo leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Shirika la GNI, Yang Jin Ok na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Madale Alex Mbuya.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik akihutubia wananchi wakati wa uzinduzi wa Shule ya Sekondari ya Maendeleo, iliyoko Nakasangwe Madale jijini Dar es Salaam iliyojengwa  kwa msaada wa kampuni ya  KIA na HYUNDAI za Korea kupitia Shirika la Good Neighbour International la Korea.

Vijana mbalimbali kutoka Shirika la GNI la nchini Korea, walioshiriki katika kujitolea kujenga Shule ya Sekondari ya Maendeleo Nakasangwe huko Madale, wakiwa katika hafla ya uzinduzi leo.

No comments:

Post a Comment