TANGAZO


Tuesday, August 21, 2012

Miss World Tanzania 2012, arejea nchini akitokea China

Mrembo Lisa Jensen ambaye ni Miss World Tanzania 2012, amerejea jijini Dar es Salaam leo, akitokea nchini China alipokwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia mwaka huu na kupokelewa na viongozi kadhaa wa Kamati ya Miss Tanzania, akiwemo Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga (kulia) aliyefika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es salaam kumpokea.
Lisa akizungumza na viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania, kutoka kushoto, Katibu Mkuu, Bosco Majaliwa, Mrembo Amisa Hassan, Mkurugenzi Hashim Lundenga na Ofisa Habari wa Kamati, Haidan Rico
Lisa akila pozi la picha na mmoja wa warembo waliofika kumpokea, Amisa Hassan. Lisa alifanikiwa kuingia Robo fainali za Top Model na kumi bora ya Shindano la Multimedia Award 2012. (SOURCE: www.mrokim.blogspot.com)

No comments:

Post a Comment