TANGAZO


Tuesday, August 7, 2012

Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal, atembelea mabanda ya maonesho ya Nanenane Dodoma


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo jinsi ya uzalishaji wa zao la zabibu kutoka kwa Ofisa Mtafiti Msaidizi wa Kilimo wa Kanda ya Kati Dodoma, Richard Malle, (wa pili kulia), wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kilimo Kwanza, kwenye maonesho ya Nanenane, Viwanja vya Nzuguni, mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012. Wa kwanza (kushoto) ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima na kulia ni Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mroso. (Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR)

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Zakhia Bilal, Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima (kushoto), wakiangalia muhogo aina ya Mumba wenye umri wa miaka 3, wakati Makamu alipotembelea katika banda la Kilimo Kwanza, kwenye maonesho ya Nanenane, Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana, Agosti 6, 2012. Wa pili kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal na wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu mbegu ya mizabibu, kutoka kwa Mkurugenzi wa Utafiti wa Kilimo, Kanda ya Kati Dodoma, Leon Mrosso (kushoto), wakati Makamu alipotembelea katika banda la Kilimo Kwanza, kwenye maonesho ya Nanenane, Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana, Agosti 6, 2012. Kulia ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal na wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. 

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi mashine ya kukamulia miwa, inavyofanya kazi, kutoka kwa jasiriamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika Banda la Kiwanda cha Sukari, kwenye maonesho ya Nanenane, Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana, Agosti 6, 2012. Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. 

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo jinsi ya uandaaji hadi kukamilika kwa sukari tayari kwa matumizi, kutoka kwa mjasiriamali, Patrisia Kisabua, wakati Makamu alipotembelea katika banda la Kiwanda cha Sukari, kwenye maonesho ya Nanenane, Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma jana, Agosti 6, 2012. Kushoto ni Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima. Wa tatu kutoka kushoto ni mke wa Makamu, Mama Zakhia Bilal. 

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiteta jambo na Naibu Waziri wa Chakula na Ushirika, Adam Malima, wakati akiondoka kwenye viwanja vya maonesho ya Siku ya Wakulima, Nanenane vya Nzuguni mjini Dodoma jana Agosti 6, 2012. 

No comments:

Post a Comment