TANGAZO


Sunday, August 12, 2012

Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal, awa mgeni rasmi mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi Qur'an Tukufu, Dar es Salaam

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2012, akiwa ni mgeni rasmi katika fainali ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tukufu Tanzania na taasisi ya Tanzania Muslim Hajj Trust, yaliyoshirikisha nchi 13, ambapo mshindi alikuwa ni Abdulrahman Salis Ahmad (18), kutoka Nigeria, aliyeshinda kwa jumla ya pointi 96.12. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
 Mmoja kati ya washiriki wanne walioiwakilisha Tanzania, katika fainali ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tukufu Tanzania na taasisi ya Tanzania Muslim Hajj Trust, yaliyoshirikisha nchi 13, Omar Abdallah, akisoma Qur-an wakati akishiriki katika fainali za mashindano hayo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2012. 

Akina baba wakiwa kwenye fainali ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tukufu Tanzania na taasisi ya Tanzania Muslim Hajj Trust, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka ukumbini wakati wa mashindano hayo leo. (Picha na Kassim Mbarouk)

Akinamama wakiwa kwenye fainali ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tukufu Tanzania na taasisi ya Tanzania Muslim Hajj Trust, wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitendeka ukumbini humo leo. (Picha na Kassim Mbarouk)


Mshiriki wa Mashindano ya kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa kutoka Kuweit, Omar Sha'ban, akisoma Qur'an Tukufu katika mashindano hayo kwa washiriki wa wanaume waliohifadhi juzuu 30, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo asubuhi. (Picha na Kassim Mbarouk)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipohudhuria na kuwa mgeni rasmi katika fainali ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tukufu Tanzania na tasisi ya Tanzania Muslim Hajj Trust, yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi ya Dola za Kimarekani 1250, mshindi wa tatu katika fainali ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tukufu Tanzania na taasisi ya Tanzania Muslim Hajj Trust, Ijaaz Mukaddam (22), kutoka Afrika ya Kusini, aliyepata jumla ya Pointi 95.08 baada ya kutangazwa washindi wa fainali hizo. Mshindi wa kwanza alikuwa ni Abdulrahman Salis Ahmad (18) kutoka Nigeria, aliyepata Pointi 96.12, wa pili ni Twalha Ally Mohammed (18) kutoka Philippines, aliyepata Pointi 96.03. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi funguo ya Pikipiki, mshindi wa kwanza kwa Watanzania, Mohammed Omar Mkilalu, baada ya kutangazwa washindi wa fainali ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tukufu Tanzania na taasisi ya Tanzania Muslim Hajj Trust, zilizofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam leo Agosti 12, 2012. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mshiriki mdogo kuliko wote katika mashindano hayo, ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tukufu Tanzania na taasisi ya Tanzania Muslim Hajj Trust, Suleyman Ahmad (9) kutoka China, aliyeshiriki akiwa amehifadhi juzuu 30 katika fainali hizo zilizofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, Ustaadh Muhammad Abdullah Balarabe, aliyeongozana na mshiriki mshindi wa kwanza katika fainali za mashindano hayo ya Kimataifa ya kuhifadhi Qur'an Tukufu, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Taasisi za Dini ya Kiislamu na washindi wa tatu Bora wa fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wakiwa katika picha ya pamoja na Majaji wa fainali za mashindano ya Kimataifa ya Qur-an, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee leo Agosti 12, 2012. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, wakiondoka katika Ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kuhudhuria fainali ya Mashindano ya Kuhifadhi Qur'an Tukufu ya Kimataifa, yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'an Tukufu Tanzania na taasisi ya Tanzania Muslim Hajj Trust, yaliyofanyika leo Agosti 12, 2012.

No comments:

Post a Comment