TANGAZO


Sunday, August 12, 2012

Alivyopokewa Dk. Ulimboka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere


Baunsa akimkinga Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, alipowasili Uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere jijini Dar es Salaam, asiguswe na hata kupigwa picha na waandishi wa habari. (Picha zote na Kassim Mbarouk na Francis Dande wa Habari mseto blog)


 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akipokewa na  madaktari pamoja na  wananchi mbalimbali, alipowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere, jijini Dar es Salaam leo, akitokea nchini Afrika Kusini alikokwenda kwa matibabu baada ya kutekwa na kupigwa na watu wasiojulikana. 
Picha hii inamuonesha Dk Ulimboka hali yake ilivyokuwa baada ya kupata kipigo na kisha kutupwa kwenye msitu wa Pande, nje ya jijini la Dar es Salaam na kisha kupelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu.

 Dk. Ulimboka akiwasili leo kutoka nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kwa matibabu huku akizongwa na mabaunsa na watu waliokuwa na shauku ya kutaka kumuona baada ya matibabu yake nchini Afrika Kusini.

Madaktari wakiwa wamemzunguka Dk. Ulimboka (katikati), pamoja na baadhi ya wananchi waliofika uwanjani hapo leo.

Dokta Ulimboka akiwa katikati ya Madaktari pamoja na wananchi waliokuwa na hamu ya kutaka kumuona, baada ya kuwasili nchini akitokea Afrika Kusini leo.

Dokta Ulimboka akijitayarisha kuzungumza na waandishi wa habari, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere, Dar es Salaam leo baada ya kuwasili nchini akitokea Afrika Kusini leo.

Dokta Ulimboka akizungumza na waandishi wa habari, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere, Dar es Salaam leo baada ya kuwasili nchini akitokea Afrika Kusini leo.
  
Dokta Ulimboka akizungumza na waandishi wa habari, uwanjani hapo leo, baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Afrika Kusini. 

Dokta Ulimboka akielekeza jambo mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, uwanjani hapo leo, baada ya kuwasili nchini akitokea nchini Afrika Kusini.  

Dokta Ulimboka akiwa ameshikilia shada la maua alilokabidhiwa na ndugu zake mara baada ya kuwasili, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere jijini leo, akitokea nchini Afrika Kusini, alikokwenda kutibiwa.  

Mwenyekiti wa Kamati ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka (kulia), akikumbatiana na Rais wa Chama cha Madaktari nchini (MAT), Dk. Namala Mkopi, mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere, jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi wa TGNP, na mwanaharakati Ussu Mallya, akinyanyua juu bango lake lenye ujumbe wa kumuunga mkono Dk. Ulimboka katika harakati zake za kudai maslahi ya Madaktari nchini. 

Mkurugenzi wa TGNP na mwanaharakati wa haki za binadamu, Ussu Mallya, akizungumza na waandishi wa habari, uwanjani hapo, wakati yeye na ujumbe wake walipokuwa wakimpokea Dk. Steven Ulimboka, alipowasili akitokea nchini Afrika Kusini leo mchana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA), Mwanaharakati Ananilea Nkya, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka, alipowasili nchini akitokea Afrika Kusini leo mchana, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere.


 Wanaharakati wakipaza sauti wakati wa mapokezi ya Ulimboka.

 Dk. Ulimboka akiwapungia mkono baadhi ya madaktari wenzake waliofika kumpokea
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akiwa ameshika ua mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, akitokea nchini Afrika Kusini kwa matibabu
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akiwa ameshika ua mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, akitokea nchini Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana. Picha ya kulia ikimuonesha Dk. Ulimboka akiwa katika hali mbaya baada ya kuokotwa katika msitu wa Mabwepande, Juni 27.


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake nchini (TAMWA), Mwanaharakati Ananilea Nkya, akisukuma gari pamoja na wananchi, madaktari na watu mbalimbali alilokuwa amepanda Dk. Ulimboka alipowasili nchini leo mchana akitokea Afrika Kusini alikopelekwa kwa matibabu baada ya kutekwa na kupigwa na watu wasiojulikana.


 Baadhi ya Wanaharakati pamoja na Madaktari wakilisukuma gari alilokuwa amepanda Dk Ulimboka mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment