TANGAZO


Sunday, August 12, 2012

Jamhuri yawatandika ndugu zao Mtende mabao 3-0

 Mchezaji Ali Mohamed Mmasai wa Mtende (kushoto), akipambana na Suleiman Ali Nuhu wa Jamhuri katika mchezo wa Ligi ya Super 8, uliochezwa Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam leo jioni ambapo Jamhuri ilishinda mabao 3-0. Mashindao hayo yamedhaminiwa na BancABC. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

 Mchezaji Ali Mohamed Mmasai wa Mtenda (kushoto), akijaribu kumpiga chenga Sadik Habib Rajab wa Jamhuri ya Pemba wakati wa mchezo huo.

 Ali Mohamed Mmasai wa Mtenda ya Unguja (kushoto), akiwania mpira na Bakari Khamis Futo wa Jamhuri ya Pemba katika mchezo huo.

 Ali Mohamed Mmasai wa Mtenda (kushoto), akimtoka Bakari Khamis Futo wa Jamhuri katika mchezo huo.

 Bakari Khamis Futo wa Jamhuri (katikati), akijaribu kuwahadaa golikipa Abdalla Suleiman Bakari (kushoto) na Lwitwiko Jackson (5) wote wa Mtende katika mchezo huo.

Bakari Khamis Futo wa Jamhuri (kulia), akijitayarisha kufunga huku akipambana na golikipa Abdalla Suleiman Bakari (kushoto) na Lwitwiko Jackson (5) wote wa Mtende katika mchezo huo.

Bakari Khamis Futo wa Jamhuri (kulia), akipiga mpira ili kufunga goli huku akizongwa na golikipa Abdalla Suleiman Bakari (kushoto) na Lwitwiko Jackson (5) wote wa Mtende katika mchezo huo.

 Golikipa Abdalla Suleiman Bakari wa Mtende, akikimbilia mpira huku ukiwa umesha wahiwa na mshambuliaji wa timu ya Jamhuri, Suleiman Ali Khatib.

 Mchezaji Ali Manzi wa Mtende akimtoka Mfaume Shaaban Ibrahim wa Jamhuri katika mchezo huo.

Mwamuzi wa mchezo huo, Hashim Abdalla akilala chini pamoja na wachezaji wa timu hizo kukwepa nyuki waliokuwa wakipita uwanjani hapo.


Mwamuzi wa mchezo huo, Hashim Abdalla akilala akiwa amelala chini pamoja na wachezaji wa timu hizo kukwepa nyuki waliokuwa wakipita uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment