Makamu Mwenyekiti wa timu ya soka ya Azam FC, Said Mohammed (kushoto), akimtambulisha kwa waandishi wa habari, Kocha mpya wa timu hiyo, Boris Bunjak katika mkutano uliofanyika, Dar es Salaam leo.
Boris Bunjak, Kocha mkuu mpya wa timu ya Azam FC, akipozi kwa picha wakati alipotambulishwa rasmi na uongozi wa timu hiyo leo, jijini Dar es Salaam, Boris Bunjak raia wa Serbia aliyezaliwa mwaka 1954, amesaini mkataba wa kuitumikia Azam FC kwa muda wa miaka miwili, Boris Bunjak amefundisha timu mbalimbali katika nchi za Kiarabu na amewahi kuichezea timu ya Taifa ya Serbia na vilabu mbalimbali huko Ulaya Mashariki, amewahi kufanya kazi pia katika Chama cha Soka cha Yugoslavia mwaka 1993-1994 na kazi nyingine nyingi kuhusiana na masuala ya soka.

Kocha Bunjak akifurahi baada ya kutambulishwa kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa timu ya Azam FC, mzee Said Mohamed Said, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kumtambulisha kocha wa timu hiyo, Boris Bunjak jijini leo.

No comments:
Post a Comment