Wapenzi ambao walifanya mapenzi nje ya ndoa wamepigwa mawe hadi kufa mwishoni mwa wiki na wapiganaji wa kiislam katika mji wa Aguelhok kaskazini mwa Mali, maafisa wamesema.
Mwanamume na mwanamke huyo walizikwa mpaka kwenye shingo na kupigwa mawe hadi kufa.
Kaskazini mwa Mali nusu yake inaendeshwa na waasi wa Tuareg na wapiganaji wa Kiislam baada ya mapinduzi katika mji mkuu wa Mali.
Aguelhok katika eneo la Kidal alikuwa ni wa kwanza kukamatwa na waasi wa Tuareg .
Waislamu katika eneo la Aguelhok waliwapiga mawe mpaka kufa watu hao mbele ya watu 200 maafisa wamesema.
"Nilikuwepo. Wapiganaji hao wa Kiislamuwaliwachukua watu hao katikati ya Aguelhok. Watu hao waliwekwa kwenye mashimo mawili na wakapigwa mawe mpaka wakafa." Afisa wa serikali eneo hilo alisema.
"Mwanamke alizimia mara baada tu ya mapigo," alisema, akiongeza kuwa mwanaume alipiga kelele mara moja tu na baadaye akanyamaza.
Uasi wa Tuareg kaskazini ulichangia mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi na kusababisha vurugu za makunbdi ya wapiganaji wa kiislam na kasha kuchukua udhibiti wa miji kadhaa ya kaskazini.
Bw Traore alisema ataongoza mazungumzo kuunda serikali ya umoja wa kitaifa nchini Mali na kuongoza juhudi za kuanzisha mazungumzo na Waislamu.
"Wananchi wa Mali hawana budi kuungana dhidi ya wavamizi,” alisema, akimaanisha wapiganaji wa kigeni wa jihadi ambao wanatuhumiwa kudhibiti eneo la kaskazini.
"Kutokana na ugumu wa mgogoro huu na ukubwa wa mateso ya watu wa Kaskazini, kwa pamoja, nasema pamoja, tunaweza kusafisha njia mbele yetu kuiweka huru nchi yetu kutoka kwa wavamizi hawa, ambao wanaacha uharibifu na huzuni, na kuwasababishia watu wetu maumivu, " alisema Bw Traore.
Kumekuwa na shutuma kutoka jumuiya ya kimataifa kwa wapiganaji wa kiislam katika mji wa zamani wa Timbuktu wakilaumiwa kwa kuharibu kumbukumbu za karne nyingi za viongozi muhimu wa dini ya Kiislam ambao wanaheshimika kwa Waislam wa madhehebu ya Sufi.
No comments:
Post a Comment