Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi za jijini Dar es Salaam, Morogoro na Singida, wakiandamana leo asubuhi kupinga hatua ya walimu kugoma kuingia madarasani kufundisha jambo ambalo wanafunzi hao wamelielezea kuwa ni kuwanyima haki zao za msingi za kuwapatia elimu, ambapo nao wamepanga kutinga Mahakamani kuwafungulia kesi walimu wao, kutokana na kile wanachodai kwamba madai ya walimu kwa Serikali, wao hayawahusu na hawahusiki kwa namna yeyote ile, alisikika mmoja wa viongozi wa wanafunzi hao aliyejitambulisha kwa jina la Shaban Mudunda.
DAR: Wananfunzi wa Shule ya Msingi Mbezi ya Jijini Dar es Salaam nao hawakuwa nyuma katika kudai haki yao ambapo nao walifikisha ujumbe kwa njia hii ya Bango, wakiwa pembezoni mwa barabara Morogoro leo asubuhi.
Nako Mkoani Singida, wanafunzi walijitokeza kwa wingi katika mitaa ya mji huo, huku wakiimba na wakiwa na baadhi ya mabango yenye ujumbe kuhusu tukio hilo, la kugoma kwa walimu.
Hawa ni Wanafunzi wa shule za msingi za Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singida. Ni katika Manispaa Singida, wakiwa nje ya Ofisi za Mkuu wa Mkoa huo leo asubuhi, ili kumfikishia ujumbe baada ya walimu wao kugoma.
No comments:
Post a Comment