Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tsn Group, Emmanuel Ngallah, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu promosheni ya Tajirika na Jambo, inayoendeshwa na Kampuni ya Jambo Concepts, kupitia gazeti lake la Jambo Leo. Amezitaja zawadi katika promosheni hiyo, kuwa ni pamoja na Bajaj yenye thamani sh. milioni 5.5, sofa set sh. milioni 2, Tv Flat screen 32' pamoja na friji lenye thamani ya sh. 650,000. Katikati ni Mkurugenzi wa Jambo Concepts, Benny Kisaka na Meneja wa kampuni hiyo, Ramadhan Kibanike.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tsn Group, Emmanuel Ngallah, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu promosheni ya Tajirika na Jambo, inayoendeshwa na Kampuni ya Jambo Concepts, kupitia gazeti lake la Jambo Leo. Amezitaja zawadi katika promosheni hiyo, kuwa ni pamoja na Bajaj yenye thamani sh. milioni 5.5, sofa set sh. milioni 2, Tv Flat screen 32' pamoja na friji lenye thamani ya sh. 650,000. Katikati ni Mkurugenzi wa Jambo Concepts, Benny Kisaka, Meneja wa kampuni hiyo, Ramadhan Kibanike (kulia) na Ofisa Mauzo na Masoko wa Tsn, Rosemary Benny.
Jambo Leo yazindua Tajirika na Jambo
Na Joyce Ngowi
KAMPUNI ya Jambo Concepts inayochapisha gazeti la Jambo Leo imeanzisha promosheni inayoitwa Tajirika na Jambo ikiwa ni moja ya kufurahia miaka mitatu tangu kuanzishwa kwa gazeti hilo na pia kuwapa wasomaji motisha kama njia mojawapo ya kuonesha kujali ushirikiano wao.
Katika kufanikisha promosheni hiyo, Jambo Concepts imeamua kushirikiana na Kampuni ya TSN Supermarkert iliyo chini ya TSN Group katika kuhakikisha wasomaji na Watanzania wengine wananufaika kwa kushinda zawadi mbalimbali kupitia promosheni hiyo inayoanza leo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Jambo Concepts, Benny Kisaka alisema katika promosheni hiyo wasomaji wa Jambo Leo, watashinda zawadi mbalimbali ikiwemo TV 'flat sreen' nchi 32, 'Laptop', 'microwave', vocha za kufanya manunuzi kwenye duka kuu la TSN (Supermarket) na kujaza mafuta katika vituo vya mafuta vya TSN vilivyo maeneo mbalimbali nchini.
Mbali ya zawadi hizo kutakuwa na zawadi kubwa ya kushinda bajaj, sofa seti, jokofu, jiko la gesi.
Kisaka alisema utoaji wa zawadi kwa washindi wa zawadi hizo utafanyika mwanzoni mwa mwezi na mwisho wa mwezi na kwamba kutakuwa na bahati nasibu kubwa baada ya miezi mitatu na mshindi atashinda bajaj.
Alifafanua kuwa bahati nasibu hiyo itasimamiwa na maofisa kutoka bahati nasibu ya Taifa ili kuhakikisha kila kitu kinakwenda kwa mujibu wa sheria na kanuni za michezo ya kubahatisha.
Alisema washiriki katika bahati nasibu hiyo ni wale ambao watakuwa na umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
Kisaka alifafanua kuwa msomaji wa Jambo Leo atatakiwa kukata kuponi itakayokuwa inapatikana ukurasa wa pili wa gazeti na kukusanya kuponi za matoleo saba mfululizo ambazo atatakiwa aziwasilishe kwa Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, SLP 3209, Dar es Salaam au aziwasilishe ofisi za gazeti hili zilizopo ghorofa ya 9 Jengo la Hifadhi, mnara wa askari makutano ya barabara ya Samora na Azikiwe na katika vituo vya mafuta vya TSN na soko kuu la TSN (Supermarket) zilizopo nchini.
Akizungumza katika uzinduzi wa promosheni ya Tajrika na Jambo Leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TSN Group , Emmanuel Ngallah alisema kuwa kampuni yao imekuwa ikijishughulisha na shuguli mbalimbali za ujenzi wa uchumi wa nchi na sasa imeona ni wakati muafaka wa kushirikiana na Jambo Concepts ili kurudisha sehemu ya faida kwa Watanzania kupitia promosheni hiyo.
Alisema TSN ni moja kati ya kampuni ambazo zimetoa ajira kwa zaidi ya Watanzania 350 na sehemu kubwa ya bidhaa wanazouza zinatoka katika maeneo mbalimbali nchini, ndiyo sababu iliyowasukuma kuona umuhimu wa kurudisha faida na kutambua mchango wa Watanzania ambao wamekuwa wakiwaunga mkono na sasa ni zamu yao kwa kuwatajirisha kupitia promosheni ya Tajirika na Jambo.
No comments:
Post a Comment