TANGAZO


Sunday, July 29, 2012

Masai Camp ya Arusha yazinduliwa upya


Wasanii wa kundi la burudani la Gotagious Danceteam Africa kutoka jijini Arusha wakitoa burudani wakati wa uzinduzi wa MASAI CAMP ya jijini humo ambayo sasa itakuwa ikitoa vionjo tofauti kwa vyakula na burudani za aina mbalimbali pamoja na vinywaji vya kila namna kwa wageni watakao kuwa wakitembelea kituo hicho cha maraha.
Wasanii wa Gotagious Danceteam Africa kutoka jijini Arusha wakitoa burudani wakati wa uzinduzi huo wa MASAI CAMP ya jijini Arusha, usiku wa kuamkia leo.
Baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Serengeti Breweries (SBL), wakipata chakula katika uzinduzi huo.
Wageni maalum katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), Teddy Mapunda (kushoto) na timu yake wakipata vyakula mbalimbali na burudani katika uzinduzi huo.

Wasanii wa kundi la burudani la Gotagious Danceteam Africa kutoka jijini Arusha wakitoa burudani wakati wa uzinduzi mpya wa MASAI CAMP, usiku wa kuamkia leo.

Wageni kutoka nje ya nchi ambao wapo jijini Arusha kwa shughuli za utalii, masomo na kazi za kujitolea, wakifuatilia burudani kutoka kundi la Gotagious Danceteam Africa la mjini humo.
Wasanii wa kundi la Gotagious Danceteam Africa, wakionesha umahiri wao mbele ya wageni mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Masai Camp ya mjini humo, usiku wa kuamkia leo.
wateja walio hudhuria katika uzinduzi huo hawakutamani burudani hiyo ikatike maana ilikonga nyoyo zao na kupata ladha ile halisi ya mahali tulivu kwa burudani na vinywaji huku misosi ikiendelea kutafunwa.

Wageni kutoka nje ya nchi, wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa na kundi la Gotagious Danceteam Africa la jijini Arusha.

Burudani ya Disco, ilikuwa ikiporomoshwa na mkali huyu kutoka majuu.

Wadau wa Masai Camp ya mjini Arusha, wakipigwa picha ya pamoja usiku wa kuamkia leo wakati wakitambulisha upya kiota hicho cha maraha.
Teddy Mapunda 'Aunt T', akishow love na mmoja wa waendeshaji wa Masai Camp katika uzinduzi huo.

Wageni mbalimbali wakizirudi ngoma za kundi la Gotagious Danceteam Africa kutoka jijini Arusha wakati likitoa burudani kwenye uzinduzi huo. (Picha zote na mpigapicha wetu)

No comments:

Post a Comment