TANGAZO


Friday, July 13, 2012

Dk. Slaa na wenzake wajisalimisha Polisi

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema wakishuka kwenye gari, mara baasa ya kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo kwa ajili ya kwenda kuhojiwa.


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema na aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema wakielekea Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo kwa ajili ya kwenda kuhojiwa.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa na mwenzake Godbless Lema wakiongozwa na Maofisa wa Polisi walipofika Makao Makuu ya jeshi hilo kwa ajili ya kuhojiwa kuhusu madai yao ya kutishiwa kuawa.

Lema akiongozwa na Oisa wa Polisi wa Makao Makuu ya jeshi hilo, kwa ajili ya kwenda kuhojiwa kuhusu madai yao ya kutishiwa kuawa.
Dk. Slaa (katikati) na wenzake wakiingia kwenye chumba cha kuhojiwa, Makao Makuu ya jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa nje ya jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi walikimsubiri Katibu Mkuu wa Chadema, Wilbroad Slaa na wenzake wakati walipokwenda kuhojiwa kuhusu tuhuma hizo leo.

Dk. Slaa, akiwapungia wanachama na wafurukutwa wa Chadema waliokuwepo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mara baada ya kutoka kuhojiwa leo na jeshi hilo.
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kutoka kuhojiwa na Jeshi la Polisi Makao Makuu ya jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo.
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa akitoka katika mahojiano yaliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
Dk. Slaa na Lema wakiwa kwenye gari lao tayari kwa kuondoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mara baada ya kumaliza kuhojiwa leo na kuzungumza na waandishi wa habari.
Baadhi ya wafurukutwa wachache wa Chama hicho, waliojitokeza Makao Makuu ya Jeshi hilo, wakilisikuma gari walilopanda Katibu wao Mkuu na Godbless Lema wakati wakiondoka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Francis Dande wa Habari Mseto)

No comments:

Post a Comment