TANGAZO


Friday, July 13, 2012

Wanafunzi 2 wa UN Clubs kuiwakilisha Tanzania Kongamano la Mandela SA



Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), Phillippe Poinsot akimkabidhi barua mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Azania, Rahim Rajab ambaye ni mmoja kati ya wanafunzi wawili, wajumbe wa UN Clubs waliochaguliwa kuhudhuria Kongamano la maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela litakalofanyika Johannesburg, Afrika Kusini ambayo huadhimishwa kila mwaka Julai 18. Wanafunzi hao wamepewa udhamini wa tiketi za kwenda na kurudi na Shirika la ndege la Afrika Kusini (South African Airways-SAA).

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP),  Phillippe Poinsot akimkabidhi barua ya kuchaguliwa kushiriki kongamano hilo nchini Afrika Kusini mwanafunzi wa kidato cha sita wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Nuru Kessy ambaye ni mwanachama wa Un Clubs.


Phillippe Poinsot, akimfafanulia mwanafunzi Nuru Kessy kuwa katika kongamano hilo, watakutana na wanafunzi wenzao kutoka mataifa mbalimbali duniani, wenye umri kati ya miaka 13-18 na kuwa wanahitaji kufanya utafiti kuhusiana na maisha ya Mandela ikiwemo miaka ya mwanzo, maisha yake ya jela, maisha ya Uraisi kama mtu aliyepokea tuzo ya amani ya Nobel, kustaafu kwake na mchango wake kama kiongozi maarufu duniani.


Wanafunzi hao wakitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP),  Phillippe Poinsot (kulia) na Mkuu wa kitengo cha Misaada na Ushirika cha UNDP, Ishmael Dodoo.


Wanafunzi ambao ni wananchama wa UN Clubs wanaoelekea Afrika Kusini katika Kongamano la maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Rais wa nchi hiyo, Nelson Mandela kwa udhamini wa Shirika la ndege la Afrika Kusini (SAA), wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa UNDP. Kushoto ni Mtunza kumbukumbu Msaidizi kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Harriet Macha, Mwambata wa kitengo cha IT,  Alice Chopeta, Mkuu wa kitengo cha Misaada na Ushirika cha UNDP, Ishmael Dodoo, wanafunzi Rahim Rajab na Nuru Kessy, Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), Phillippe Poinsot na Ofisa habari wa UNIC, Stella Vuzo. (Picha zote na mdau wetu)

No comments:

Post a Comment