Baadhi ya Wanasheria wa Chama cha Tanganyika Law Society, wakiwa kwenye hafla ya kuuaga mwili wa Mwanasheria mwenzao, marehemu Bob Mohamed Makani, viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo mchana.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu na kukusanya maoni ya Katiba Mpya, Jaji Sinde Warioba, akiwasili na mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo, Salim Ahmed Salim (kulia), kwenye viwanja vya karimjee kwa ajili ya kuuaga mwili huo.
Mjumbe wa Kamati ya Kuratibu na Kukusanya maoni ya Katiba Mpya, Salim Ahmed Salim (kulia), akizungumza jambo na mke wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, Anna, wakati wa hafla ya kuuaga mwili wa marehemu Bob Makani viwanjani hapo leo.
Mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhwan Kikwete, akiwasili viwanjani hapo kwa ajili ya kuuaga mwili huo, huku akilakiwa na mmoja wa vijana wa Chadema.
Baadhi ya wananchi, viongozi wa Chadema na waombolezaji kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es Salaam, wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kusubiri kuuaga mwili wa marehemu Bob Makani.
Baadhi ya Wanasheria wa Chama cha Tanganyika Law Society, wakiwa kwenye hafla ya kuuaga mwili wa Mwanasheria mwenzao, marehemu Bob Mohamed Makani, viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam leo mchana, ambapo mwili wake baadaye ulitegemewa kupelekwa Uwanja wa ndege wa JK Nyerere kwa ajili ya kusafirishwa kesho asubuhi kupelekwa kwao Shinyanga kwa ajili ya mazishi.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad (kulia), akiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, wakiwasili viwanjani hapo kwa ajili ya kuuaga mwili huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad (wa pili kushoto), akilakiwa na Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi na Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe (kulia), wakatai alipofika katika viwanja hivyo na Mwenyekiti wake Profesa Lipumba (kushoto) kwa ajili ya kuuaga mwili wa Bob Makani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad (kushoto), akimpa pole Naibu Katibu Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe, wakati alipowasili viwanjani hapo kuuaga mwili huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad (kushoto), akisalimiana na Rais Jakaya Kikwete, alipowasili viwanjani hapo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa.
Baadhi ya viongozi, wananchi na waombolezaji wakiwa kwenye viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kuuaga mwili wa Bob Makani leo.
Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal (katikati), akiwa na mke wa Rais Kikwete, mama Salma (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Slaa, viwanjani hapo wakati wa kuuaga mwili huo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad (katikati), akiwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kuratibu na kukusanya maoni ya Katiba Mpya, Jaji Sinde Warioba katika hafla ya kuuaga mwili huo, jijini leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama (kushoto), wakati wa kuuaga mwili huo leo, viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Dar es Salaam.
Jenenza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa mwanzilishi wa Chadema, marehemu Bob Mohamed Makani, likitolewa kwenye gari, wakati lilipoletwa viwanjani hapo kwa ajili ya kuuaga mwili wa marehemu Bob Makani.
Baadhi ya Wanasheria wa Chama cha Tanganyika Law Society, wakiwa pamoja na baadhi ya wafurukutwa wa Chadema, wakilibeba jenenza lililokuwa na mwili wa marehemu Bob Makani kwa ajili ya kuuweka kwenye viwanja hivyo tayari kwa kuuaga leo mchana.
Rais Jakaya Kikwete (katikati), akiwa na Makamu wake, Gharib Mohamed Bilal (kulia) na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe (kushoto), wakilibeba jenenza lililowekwa mwili wa aliyekuwa muanzilishi wa Chama hicho, marehemu Bob Mohamed Makani, wakati wa kuuaga mwili wake, viwanja vya Karimjee Dar es Salaam leo mchana.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, akizungumza katika hafla ya kuuaga mwili huo.
Rais Jakaya Kikwete, akizungumza kwa ajili ya kutoa salamu zake za rambirambi wakati wa hafla ya kuuaga mwili huo leo mchana.
Rais Jakaya Kikwete na mkewe, mama salma wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu Bob Makani wakati wa kuuaga mwili huo, viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete akiwapa mkono wa pole watoto na wajukuu wa marehemu Bob Makani wakati wa kuuaga mwili huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akiwapa mkono wa pole watoto na wajukuu wa marehemu Bob Makani wakati wa kuuaga mwili huo.
Rais Jakaya Kikwete akiwa na Makamu wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal (wa pili kushoto), makamu wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad (wa tatu kushoto), mama Salma Kikwete (kulia) pamoja na viongozi mbalimbali wa Vyama vya siasa na Kamati ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya, wakiomba dua ili kuuombea mwili wa marehemu Bob Makani kabla ya kusafirishwa kupelekwa kwao Shinyanga kwa ajili ya mazishi kesho.
No comments:
Post a Comment