TANGAZO


Tuesday, June 12, 2012

Waziri Mkuu Pinda na matukio ya kuapishwa wabunge wapya Dodoma leo


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda,  akizungumza na  Mbunge wa Viti Maalum, Pauline Gekul na watoto wake Irene (kushoto)  na Inocentia, kwenye viwanja vya Bunge, mjini Dodoma leo,  Juni 12, 2012. (Picha zote na Ofisi  ya Waziri Mkuu) 
Spika wa Bunge, Anne Makinda akimkabidhi kanuni za Bunge Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia baada ya kumuapisha, Bungeni mjini Dodoma, leo Juni 12,2012.
Mbunge wa Kuteuliwa, Janet Zebedayo Mbene, akiapa Bungeni, mjini Dodoma  leo Juni 12, 2012. Mbene baada ya kuteuliwa kuwa mbunge, aliteuliwa na Rais Jakaya Kikwete, kushika nafasi ya Naibu Waziri wa Fedha.
Mbunge wa kuteuliwa, Saada  Mkuya Salum, akiapa Bungeni mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa pili kushoto), akizungumza na Wabunge kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo. Kushoto ni Vita Kawawa wa Namtumbo.

Mbunge wa kuteuliwa, Sospeter  Mwijarubi Muhongo, akiapa Bungeni mjini Dodoma, leo Juni 12, 2012. 

No comments:

Post a Comment