TANGAZO


Monday, June 11, 2012

Tamsha la uzinduzi na utambulisho wa Airtel Super 5, Iringa

Wasanii chipukizi wa muziki wa bongo fleva, waitwao Wavuka Boada, wakilishambulia jukwaa mbele ya umati wa wakazi wa Iringa waliojitokeza kwa wingi jana jioni kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa, mjini humo, wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya Airtel Supa5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za mawasiliano kupitia Airtel. Huduma hiyo itaendelea kutambulishwa tena katika Mkoa wa Arusha na baadaye Mwanza.


Mmoja wa wakazi wa Iringa aitwaye Theresia Mifwa, akikabidhiwa simu ya mkononi aina ya sumsung na Meneja Mahusiano wa  Airtel-Tanzania, Jackson Mmbando, mara baada ya kuichambua vyema huduma ya Jiunge na Supa5 kwa ufasaha, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5, uliyofanyika jana, Uwanja wa Mwembe Togwa mkoani Iringa. Airtel Jiunge na Supa5 Ilizinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Ukitaka kujiunga na huduma hiyo ANDIKA SMS YENYE NENO ‘WIKI’  AU WIKI UTUME KWENDA 15548.


Kundi la wasani wa muziki wa kizazi kipya, lenye maskani yake Temeke, jijini Dar es Salaam, la Wanaume Halisi, likiongozwa na Sir Juma Nature (kulia), wakilishambulia jukwaa vilivyo jana jioni mbele ya wananchi wa Iringa waliojitokeza kwa wingi uwanja wa Mwembe Togwa, mjini humo na kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Supa5. 


Msanii Juma Nature wa kundi la Wanaume Halisi, akilishambulia jukwaa  jana jioni mbele ya wakazi wa Iringa waliojitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Mwembe Togwa, mjini humo kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel.


Kundi la wasani wa muziki wa kizazi kipya, lenya makazi yake Manzese jijini Dar, likiongozwa na Madee,Tunda Man na wengineo, wakilishambulia jukwaa jana jioni, mbele ya umati wa wakazi wa Iringa waliojitokeza Uwanja wa Mwembe Togwa, mjini humo, kushuhudia uzinduzi wa huduma hiyo.


Sehemu ya wakazi wa Iringa waliofurika jana kwenye uwanja wa Mwembe Togwa wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya airtel Supa 5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel wakifurahia burudani iliyokuwa ikitolewa kwenye uzinduzi huo jana jioni.


Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya (hip hop), aitwaye Roma, akiwarusha wakazi wa mji wa Iringa walijitokeza kwa wingi Uwanja wa Mwembe Togwa, mjini humo kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa 5.


Kundi la wasani mahiri wa muziki wa kizazi kipya, lenya makazi yake Manzese jijini Dar, likiongozwa na Madee, Tunda Man na wengineo, wakilishambulia jukwaa vilivyo jana jioni mbele ya umati wa wakazi wa Iringa waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Mwembe Togwa, mjini humo, wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Supa 5.



Wakazi mbalimbali wa mjini Iringa wakiendelea kuhamia Airtel na kujipatia huduma mbalimbali zilizokuwa zikipatikana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Supa 5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel kwa wateja wake jana jioni. (Picha na Mdau wetu)

No comments:

Post a Comment