Balozi Celestine Joseph Mushy, akila kiapo mbele ya Rais jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam, wakati wa hafla hiyo.
Balozi Dora Mmari Msechu, akiapa mbele ya Rais Jakaya Kikwete, kuwa mwaminifu kwake na Taifa pia katika kutekeleza jukumu lake la uongozi katika sehemu yake ya kazi wizarani hapo.
Balozi Hassan Simba Yahya, akiapa kuwa mwaminifu na utiifu kwa Rais, Taifa na pia katika kutekeleza majukumu yake mapya aliyokabidhiwa na Rais Kikwete, wakati wa hafla ya kuwaapisha Mabalozi kumi kushika uongozi katika Idara na Kurugenzi mbalimbali za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ikulu jijini leo.
Balozi Irene Mkwawa Kasyanju, akiapa mbele ya Rais Kikwete katika kutekeleza majukumu yake mapya aliyomkabidhi wizarani hapo.
Rais Jakaya Kikwete akimuapisha Balozi Mbelwa Brighton Kairuki katika hafla hiyo, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Balozi Naimi Sweetie Hamza Aziz, akiapa mbele ya Rais Kikwete katika kuyatekeleza majukumu yake mapya aliyomkabidhi.
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi, akiapa kwa nafasi aliyokabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete (kushoto), wakati wa hafla ya kuwaapisha Mabalozi hao, Ikulu jijini leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Balozi Silima Kombo Haji katika hafla hiyo, Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Balozi Vincent Joel Thomas Kibwana, akila kiapo cha utiifu na uaminifu kwa Rais Kikwete, Taifa na katika kutekeleza majukumu yake mapya aliyokabidhiwa naye.
Rais akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya aliowaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Kutoka kushoto waliosimama mstari wa mbele ni Balozi Bertha Semu Somi, Balozi Hassan Simba Yahya, Balozi Vincent Joel Thomas Kibwana, Balozi Naimi Sweetie Hamza Aziz, Balozi Irene Mkwawa Kasyanju na Balozi Dora Mmari Msechu. Waliosimama nyuma kutoka kushoto ni Balozi Silima Kombo Haji, Balozi Celestine Joseph Mushy, Balozi Mbelwa Brighton Kairuki na Balozi Ramadhan Muombwa Haji (Picha na Freddy Maro)
No comments:
Post a Comment