TANGAZO


Monday, June 11, 2012

Waziri Fenella, afungua Kikao kazi cha Maofisa Habari Mwanza

Waziri wa Habari, vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella  Mukangara akiongea na Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali leo, jijini Mwanza. Pamoja na mambo mengine amewataka maafisa hao kuielimisha jamii kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo yanayofanywa na Serikali kupitia vyombo vya habari.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Seith Kamuhanda (mstari wa kwanza mbele), akifuatilia mada  kuhusu changamoto zinazoikabili Tanzania katika kuhama kutoka mfumo wa Analojia  kwenda Digitali kufikia mwaka 2012 katika Kikao kazi cha Maafisa habari na Mawasiliano wa Serikali leo, jijini Mwanza. Wengine wanaoonekana nyuma ni Maofisa habari na Mawasiliano wa Serikali.


Maofisa Habari na Mawasiliano wa Serikali, wakifuatilia kwa makini hotuba  iliyokuwa ikitolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo leo jijini Mwanza.


Waziri wa Habari, Vijana na Utamaduni Dk. Fenella Mukangara (mstari wa kwanza katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Wizara hiyo na Maofisa habari na Mawasiliano wa Serikali, mara baada ya kufungua kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano leo jijini Mwanza. (Picha na Aron Msigwa – MAELEZO)

No comments:

Post a Comment