Bingwa wa Dunia wa uzani wa welter tawi la masumbwi la WBO Manny Pacquiao amepoteza taji lake kwa mara ya kwanza aliposhindwa na Mmarekani Timothy Bradley kufuatia uwamuzi wa kutatanisha mjini Las Vegas.
Licha ya Pacquiao kupiga ngumi 94 ikiwa ni zaidi ya mpinzani kiwango cha kwake, Mfilipino huyo alishindwa kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka saba baada ya waamuzi wawili kuamua kuwa Timothy Bradley ameshinda kwa 115-113, uwamuzi uliegemea hilo.
Mwamuzi mwingine alitofautiana na wenzake akimpa ushindi Pacquiao wa 115-113.
Watazamaji wa pambano hilo hawakuridhika na uwamuzi uliotangazwa na walizomea sana baada ya Bradley kutangazwa kua mshindi na hilo limezua uwezekano wa pambano la marudio baadaye mwaka huu.
"nilihisi nimeshinda," alisema Bradley, ambaye hapo kabla alikua amechapisha tiketi kabambe za kuonyesha pambano la marudano kufanyika tarehe 10 novemba.
Bradley aliongezea kusema kua "sidhani ni hodari kama wengi walivyomsifu. Makonde yake hayakua na nguvu."
Pacquiao alichelewa kuingia ukumbini lakini alipoingia alianza raundi ya kwanza kiuzembe uzembe ingawa alirusha ngumi tatu katika sekundi za mwisho wa raundi.
Hadi kufikia raundi ya tano Bradley alionekana kuzidiwa kutokana na maumivu ya jeraha la kidole cha mguu ikionekana kua Pacquiao anaelekea kupata ushindi wa mteremko.
Kwa upande wa Bradley alifanya vizuri katika raundi tatu za mwisho lakini watazamaji hawakuridhika na hilo.
Promota wa masumbwi, Bob Bradley alisema haiaminiki. Aliongezea kusema kua punde baada ya pambano kumalizika, alikwenda kwake Bradley na akamwambia, Nimejitahidi kadri ya uwezo wangu lakini sikuweza kumshinda mtu huyo.'"
Pacquiao mwenyewe alisema hakuweza kuamini matokeo hayo. Aliongezea kua nimejitahidi lakini naona juhudi zangu hazikutosha.
Ngumi zake hazikunidhuru, mara nyingi ngumi zake ziliishia kwenye mikono yangu.alisema Pacquiao.
No comments:
Post a Comment