Ripoti kutoka Damascus zinaonesha mapambano makali baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa upinzani katika mji mkuu.
Walioshuhudia matukio hayo wanasema wapiganaji wa Jeshi Huru la Syria walifanya mashambulio yaliyopangwa dhidi ya vituo vya serikali siku ya Ijumaa.
Kinu cha umeme kilishambuliwa na moshi ulionekana.
Basi lilobeba wafanyakazi wa sekta ya mafuta kutoka Urusi lilipigwa.
Mashahidi wanasema wapiganaji wengi waliohusika waliuwawa au kukamatwa.
Haijulikani jeshi la serikali lilipata hasara gani na wakuu mjini Damascus hawakusema kitu juu ya tukio hilo.
Huku nyuma Baraza la kitaifa la Syria (SNC) limemchagua mwanaharakati mwenye asili ya Ki-Kurdi kama Rais wake mpya.
Abdelbaset Sayda alichaguliwa kuchukua pahala pa Burhan Ghalioun, aliyeshikilia wadhifa huo tangu kundi hilo liundwe mnamo mwezi Septemba.
No comments:
Post a Comment