TANGAZO


Sunday, June 10, 2012

Waziri Kagasheki apokelewa kishujaa Bukoba


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Bukoba, Cositancia Buhiye akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Sued Kagasheki, alipowasili uwanja wa ndege mjini Bukoba leo.

 Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anathory Amani, akimkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki alipowasili uwanja wa ndege, mjini Bukoba leo.

 Sheikh wa Wilaya ya Bukoba Sheikh Haruna kichwabuta akimsalimia na kumkaribisha nyumbani Waziri wa maliasili na Utalii, Balozi Kagasheki, alipowasili uwanja wa ndege, mjini humo leo.

 Baadhi ya wananchi wa Bukomba mjini, wakimlaki kwa mapokezi ya nguvu nje ya uwanja wa ndege, Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Hamis Kagasheki, alipowasili mjini humo leo.

Mamia ya wananchi wa Bukoba mjini, waliofika kumlaki Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Hamis Sued Kagasheki, wakisalimiana naye nje ya Uwanja wa ndege wa mjini Bukoba leo, mara baada ya kuwasili mjini humo. (Picha kwa hisani ya Bukobawadau Blog)

No comments:

Post a Comment