TANGAZO


Sunday, June 10, 2012

Stars yaiadhibu Gambia, yaitandika 2-1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Kikosi cha timu ya Taifa, Kilimajaro Taifa Stars, kipiga picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu ya mchezo wao na Gambia, kuwania kufuzu kwa kombe la dunia 2014, mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.

Kikosi cha timu ya Gambia kikipiga picha hiyo ya kumbukumbu, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo jioni.

 Mashabiki wa timu ya Taifa, Kilimanjaro Taifa Stars, wakifuatilia mchezo baina ya timu hiyo na Taifa ya Gambia, mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni.


 Mchezaji Mbwana Samatta wa Stars, akiwa ameangushwa chini na wachezaji wa gambia, waliokuwa wakijaribu kumnyang'anya mpira wakati akiwatoka kuelekea kwenye lango lao.


 Ubao wa matokeo, ukionsha goli la Gambia, lililopatikana katika dakika ya saba ya mchezo, lililofungwa kwa kichwa na mshambuliaji wao mrefu Mustapha Jarju.


 Mbwana Samatta wa Stars, akiupiga kichwa mpira wa juu, mbele ya wachezaji Osman Koli (kushoto) na Pamodou Jagne wa gambia.


Mbawana Samatta wa Kilimanjaro Taifa Stars (katikati), akijaribu kuwatoka Yankuba Ceesay (kushoto) na Momoduou Ceesay wa Gambia, katika mchezo huo, Uwanja wa Taifa jijini, Dar es Salaam leo jioni.


Mbawana Samata (kulia), akiwagonganisha wachezaji ndugu wa Gambia, Yankuba Ceesay (kushoto) na Momoduou Ceesay (katikati), katika mchezo huo.


 Ubao wa matokeo, ukionesha bao 1-1, baada ya Stars kusawazisha kupitia mpira wa Shomari Kapombe katika dakika ya 65 ya mchezo huo.


 Mashabiki wa upande wa jukwa la Yanga, wakifuatilia mchezo huo, ambao leo kwa mara ya kwanza walionekana kuwa wazalendo kwa kuikubali Stars na kuishangilia kwa nguvu zote.


 Mbwana Samatta wa Stars, akipiga mpira mbele ya Abdou Jammeh wa Gambia katika mchezo huo.


Mbwana Samatta (kushoto), akipongezwa na Haruna Moshi na Salum Abubakar baada ya kusababisha penalt, ambayo baadaye ilipigwa na Erasto Nyoni na mpira kujaa wavuni na kuwa goli la pili kwa Stars na matokeo kudumu hadi mwisho wa mchezo Stars 2 Gambia 1.


 Golikipa wa Gambia, Musa Kamara akidaka bila mafanikio mpira (kulia) wa penalti uliopigwa na Erasto Nyoni wa Stars katika mchezo huo.


 Nyoni na Samatta wa Stars, wakishangilia bao hilo la pili lililopatikana kwa mkwaju wa penalti alioupiga na kumshinda golikipa Musa Kamara.


Nyoni na Samatta wa Stars, wakikimbia pamoja hadi kwenye jukwa la mashabiki wa Yanga kwa ajili ya kushangilia bao hilo.


Samatta akimminya Nyoni, akama ishara ya kuinyonga Gambia kwa penalti hiyo, iliyopigwa na Nyoni. 


 Mashabiki wa jukawa la Yanga, wakishangilia goli hilo, baada ya kuwekwa kimiani kifundi na Erasto Nyoni wa Stars.


 Refarii Ruzive Ruzive, akimhimiza Nyoni kurudi uwanjani kwa ajili ya kuendelea na mchezo baada ya kushangilia goli lake hilo la penalti.


 Hadi dakika hiyo ya 85, ubao wa matokeo Uwanjani hapo, ulikuwa ukisomeka Taifa Stars 2 The Scorpions 1.


Makocha wa Stars Kim Poulsen (kulia) na wa Gambia Luciano Mancini, wakipena mikono na kuzungumza kwa kupongezana kwa mchezo huo.


 Kocha Poulsen wa Stars (kulia), akimsikiliza wa Mancini wa Gambia, baada ya kumalizika kwa mchezo huo.

 Wachezaji wa Stars wakitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo huo na kuibuka kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam leo na hivyo kushika nafasi ya pili ya kundi lao, linaloongozwa na Ivory Coast.


 Wachezaji wa Stars, Haruna, Messi na Nyoso, wakizungumza kwa furaha wakati wakitoka uwanjani kwenye mchezo huo. 


 Kapteni wa Stars, Juma Kaseja akitoka kuwapongeza mashabiki wa jukwa la Yanga kutokana na kuwaunga mkono kwenye mchezo huo, walioshinda mabao 2-1.


 Kocha wa Stars Kim Pousen, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika mchezo huo na kuwasifu wachezaji wake ambapo pia hakusita kueleza mapungufu yao, lakini akaeleza kuwa ataendelea kuayafanyia kazi na kueleza kuwa ubora wa mchezaji na mchezaji mwenyewe haununuliwi dukani bali ni kwa njia hiyo ya kurekebisha makosa kila yanapotokea. Kulia ni Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura.


Kocha wa Gambia Luciano Mancini, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo, ambapo aliisifu upigaji wa penalti ya Stars na mchezo uliooneshwa na timu hiyo kwenye mchezo na timu yake ya Gambia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo jioni. Kulia ni Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura. (Picha zote na Kassim Mbarouk)

No comments:

Post a Comment