Redds Miss Chang’ombe 2012, Catherine Masumbigana 21 (katikati), akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia leo. Kulia ni mshindi wa pili, Jesca Haule (18) na Mshindi wa tatu Zulfa Bundala. Masumbigana aliwashinda warembo wengine 13 katika shindano, lililofanyika katika Ukumbi wa Quality Center jijini Dar es Salaam Juni 10, 2012.
Tano bora ya Miss Chang’ombe 2012, ambao wote wamepata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Temeke 2012, wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka Kushoto ni Zulfa Bundala (14), Jesca Haule (2), Catherine Masumbigana (10), Miriam Nkisigwa (8) na Flora Kazungu (7), wakiwa wamepozi.
Warembo wakicheza show maalum ya ufunguzi wa kinyang'anyiro hicho. ( Picha na Mroky Mroky wa FATHER KIDEVU BLOGSPOT)
Baadhi ya washiriki wa shindano hilo, wakipozi wakati walipokuwa wakipita kwenye jukwaa na vazi la kubuni.
Washiriki wakionesha vazi la ufukwenu, wakati wa kinyang'anyiro hicho, ukumbini hapo. Kutoka kulia ni Restituta Faustiney, Wensley Mabula na Clara Diu.
Baadhi ya warembo wa Shindano la Miss Chamg'ombe, Flora Mayasa (kulia), Catherine Masumbigana (katikati) na Elizabeth Mushi, wakipita na vazi la ufukweni.
Msanii bingwa wa miondoko ya Bongo Fleva, Nassib Abdul 'Diamond' akionesha manjonjo yake, wakati alipokuwa akitumbuiza na vijana wake kwenye shindano hilo, ukumbini hapo.
Mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo (Mb), Amos Makala akizungumza kwenye shindano hilo. (Picha na Fullshangwe Blogspot)
No comments:
Post a Comment