Katibu na Msemaji wa Umoja wa Wafanyabiashara Wamachinga wa Kariakoo, Patrick Mussa, akisoma risala ya wafanyabiashara hao kwa Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', wakati walipomwita kwa ajili ya kumweleza matatizo yanayowakabili kwenye biashara zao katika maeneo yao hayo. (Picha na Kassim Mbarouk)
Baadhi ya Wafanyabiashara wakimachinga wa Kariakoo, wakisikiliza masuala mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wao kwa Mbunge wao, Mussa Azzan 'Zungu', wakati walipomwita kwa ajili ya kumweleza matatizo yanayowakabili kwenye biashara zao katika maeneo yao hayo.
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akitoa ufafanuzi kwa wafanyabiashara hao, wakati alipokuwa akiwasikiliza matatizo wanayokabiliana nayo kwenye biashara zao katika sehemu zao za kufanyia biashara. Katikati ni Diwani wa Kariakoo Abdulkarim Masamaki.
Mfanyabiashara Stephen Lusinde, akitoa malalamiko yake kuhusu matatizo yanayowakabili kwenye biashara zao katika sehemu hiyo.
Mfanyabiashara Arnold Dismas, akielezea matatizo yanayowakabili kwenye eneo lao la biashara, ambapo alidai kwamba wamekuwa wakisumbuliwa na Mgambo wa Manispaa kwa kuchua bidhaa zao na kisha kupelekwa Mahakamani.
Mfanyabiashara Omar Bakari, akitoa malalamiko yake kwa Mbunge Zungu, kuhusu matatizo yanayowakabili wafanyabiashara hao kwenye biashara zao katika sehemu hiyo.
Mfanyabiashara Theobold Masawe, akitoa malalamiko yake kuhusu matatizo ya kunyang'anywa bidhaa zao na Mgambo wa Jiji kwenye biashara zao katika sehemu hiyo kwa Mbunge Zungu leo wakati alipokuwa akiwasikiliza kuhusu matatizo yao kwenye kazi zao.
Diwani wa Kariakoo Abdulkarim Masamaki, akizunguma na wafanyabiashara hao na kuwataka kufafanua zaidi kuhusu matatizo yao hayo, wakati wa mkutano huo wa Mbunge Zungu (katikati), jijini leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Dickson Fidelis.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Dickson Fidelis, akimweleza kuhusu matatizo hayo, wakati alipomtaka kufafanua zaidi juu ya maeneo wanayofanyia biashara zao na ambayo wao wanayalalamikia kuchukuliwa bidhaa zao na mgambo wa Manispaa ya Ilala. Katikati ni Mbunge wao, Mussa Azzan 'Zungu'.
Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akizungumza na wafanyabiashara hao, mara baada ya kuwasikiliza matatizo yanayowakabili katika sehemu zao za kazi, Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Diwani wa Kariakoo, Abdulkarim Masamaki, kushoto ni Mwenyekiti wa wafanyabiashara hao, Dickson Fidelis na kulia ni Katibu wake na Msemaji wa Umoja wa wafanyabiashara hao, Patrick Mussa.
Katibu wa Vijana wa Kata ya Mchikichini Baghadad, Agata Daud, akielezea matatizo yao yanayowakabili kwenye mtaa wao huo, kwa Mbunge Zungu, ikiwemo ubovu wa miundombinu isiyokidhi matakwa ya eneo hilo pamoja na mambo mbalimbali ya kimaendeleo katika mtaa huo.
Diwani wa Kata ya Mchikichini, Gharib Riyami, akifafanua kuhusu baadhi ya hatua ambazo alishaanza kuzichukua katika kukabiliana na baadhi ya kero hizo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', akisikiliza hatua hizo.
Kijana wa Mchikichini Baghadad, Stephano Daud, akimweleza Mbunge Zungu hatari zinazowakabili kutokana na kukosekana kwa baadhi ya miundombinu inayokidhi kwenye maeneo yao hayo ya makazi, ambapo alisema ni pamoja na kuziba kwa mifereji ya kupitishia maji taka na ya mvua.
Mbunge Zungu akizungumza na vijana hao, kuhusu njia na hatua ambazo atazichukua kwa kushirikiana nao katika kutatua matatizo yao hayo na pia njia ya kuwasaidia katika kuwapatia maendeleo, ikiwemo kusaidia miradi yao ya Maendeleo. Kushoto ni Diwani wa Kata ya Mchikichini, Gharib Riyami, wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Mtaa huo, Said Walala na kulia ni Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Mchikichini, Matilda Kihemka.
Mbunge Zungu akizungumza na vijana hao, kuhusu njia na hatua ambazo atazichukua kwa kushirikiana nao katika kutatua matatizo yao hayo na pia njia ya kuwasaidia katika kuwapatia maendeleo, ikiwemo kusaidia miradi yao ya Maendeleo.
Baadhi ya vijana wa Kata ya Mchikichini Baghadad, wakimsikiliza Mbunge wao, Mussa Azzan 'Zungu', wakati wa mkutano wao huo, jijini Dar es Salaam leo.
No comments:
Post a Comment