Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumanne Maghembe, akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika Viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo kwa ajili ya kutoa msimamo kwa masuala kadhaa yakiwemo matatizo ya usafiri, barabara, makazi na maji. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Umati wa wananchama na wananchi waliojitokeza katika mkutano huo wa hadhara, viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam leo, ukinyosha mikono ili kukubaliana na hotuba za viongozi wao.
Katibu wa Halimashauri Kuu, Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nauye, akiteta na Kada wa chama hicho, Stephen Wasira na Anna Tibaijuka kwenye mkutano huo, Jangwani leo.
Baadhi ya wakereketwa wa Chama hicho, wakifurahia houba za viongozi wao kwenye mkuatano huo, Jangwani Dar es Salaam leo.
Kada wa CCM, Stephen Wasira, akihutubia kwenye mkutano huo, wakati alipopata nafasi ya kuzungumza Uwanjani hapo leo.
Umati wa wanachama wa Chama hicho waliojitokeza kwenye mkutano huo, wakisikiliza hotuba za viongozi wao kwenye mkutano huo, uliokuwa umejaza wafusi wa chama hicho.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdurahaman Kinana (kushoto), akimpongeza Stephen Wasira kwa hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano huo Jangwani leo.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Harrison Mwakyembe, akihutubia mkutano huo, wakati alipokuwa akitoa nasaha zake kwa wanacha wa Chama hicho.
Baadhi ya wanachama wa Chama hicho, wakiwa wameshikilia bendera za Chama hicho kwenye mkutano hu, Jangwani Dar es Salaam leo.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi, Anna Tibaijuka, akihutubia kwenye mkutano huo na kuwaeleza wananchi na Wtanzania wote kwa ujumla kwamba hakuna mwananchi yeyote atayevunjiwa nyumba bila ya kulipwa fidia, wakati wa mkutano huo wa Jangwani, Dar es Salaam leo,
Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita (kushoto), akiteta jambo na Kada mwenzake, John Magufuli, wakati wa mkutano huo jijini leo.
Baadhi ya viongozi wa CCM, wakiimba na kupiga makofi wakati baadhi ya wanachama walipokuwa wakirejesha kadi, bendere, na vifaa vingine.
Baadhi ya viongozi wa CCM Taifa, wakichambua kadi zilizrojeshwa na wananchama wa vyama vya upinzani kwenye mkutano huo, Jangwani Dar es Salaam leo.
Kijana Mkereketwa wa CCM, akipuliza Vuvu zela lake,wakati wa mkutano huo Jangwani leo.
Baadhi ya wanachama na wakereketwa wa Chama hicho, wakicheza ngoma za kitamaduni wakati wa mkuano huo wa hadhara, Jangwani jijini Dar es Salaam leo.
Waimbaji wa kundi la sanaa la Tanzania One Theatre, wakiimba nyimbo za kuhamasisha vijana wakati wa mkutano huo, uliokuwa umejaza watu isivyo kawaida.
No comments:
Post a Comment